Fursa zinavyotupita watanzania kwa uvivu wetu na uchoyo wetu na uoga wetu wa kuzichangamkia

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Habari zenu wakuu.

Katika pita pita zangu nimekutana na kitu mitandaoni kimenishtusha sana.

Kumekuwa na fursa nyingi sana za fedha zimekuwa zikitangazwa kwa ajili ya wajasiriamali kutoka nje ya nchi maalumu kwa watu wetu wa ukanda huu wa AFRIKA MASHARIKI na kwa WATANZANIA lakini nyingi Watanzania tumekua hatuonekani tukizichangamkia.

Nyingi ya fursa hizo zimekua ni BUSINESS IDEA COMPETIOTIONS, MIKOPO(LOANS), MISAADA(GRANTS), FEDHA YA KUANZISHIA MRADI(SEED FUNDS) na nyingine nyingi ambazo zinazohitaji mjasiriamali uzichangamkie, lakini katika analysis yangu nimegundua mambo makuu matatu:
  1. Vijana wengi wa Kikenya na Kinyarwanda wamekuwa wakichangamkia sana fursa hizi na wanazipata kweli kweli kitu kunachopelekea mpaka baadhi ya watoa fedha hao ku-limit idadi ya Wakenya wanaotuma applications kwa ajili ya fursa hizo, mfano fursa inaweza kutangazwa na ikawa inataka vijana say 20 kutoka East Africa, utakuta tangazo linasema "we only receive a maximum of 10 applications from Kenya and Rwanda", lakini pamoja na hayo bado hakuna Mtanzania atakaye omba mpaka deadline itapita.
  2. Fursa nyingi ambazo zinakua zimelenga kwa wajasiriamali wa Kitanzania nyingi zinaongezewa deadlines kutokana na kuokufanyiwa applications i.e haziombwi hivyo nyingi zina extendiwa deadlines, lakini pamoja na hayo bado applications zinakua chache sana.
  3. Wajasiriamali wengi wa kitanzania hawana habari au ni waoga kutafuta habari kutoka vyanzo vya nje, na hata kama wakizipata wengi ni waoga kutuma applications, tendency hii nimeiona pia kwa Burundi na Uganda pia, lakini Wanyarwandwa na Wakenya wako sharp sana.

Kwa kuwa tuna jukwaa hili la biashara na ujasiriamali nafikiri ni vizuri mtu akipata fursa mahali ambayo ni ya kutoa mkopo(LOAN), au msaada(GRANT) au kianzio cha mradi(SEED FUND) au business idea competition ni vizuri akaiweka hapa jukwaani ili angalau tujaribu na sisi kama wenzetu Wakenya na Wanarwanda wanavyozichangamkia fursa kwa tabia yao ya kutopenda kulegea legea na kupenda kuthubutu.

Binafsi nimeamua kila week nitakua nina-POST hapa jukwaani angalau nyuzi 3 za fursa yoyote iliyojitokeza inayotulenga Watanzania ili angalau tuamke maana tumelala mno.

NB:
Ikibidi uwepo uzi maalumu ambao ni STICKY ambao mtu yeyote akipata fursa yoyote iwe ni ya kilimo au biashara au ufugaji anaipost ili kila mtu aione na kama kujaribu ajaribu kwa kuwa karibu applications zote zinafanyika online.

Mungu awabariki.
 

Well said Asigwa
 
Kwa mfano ni grant gani umeshawahi kuiona?
Maana mi naona maruweruwe tu
 
UMENENA wakenya wanauza MAUA TOKA ARUSHA-TZ, HOTEL ZA KITALII WAKENYA, SUPERMARKET WAKENYA Fursa nyingi wamezidaka "

TATIZO TZ ELIMU, WENZETU WAKIWA CHUO ELIMU YA UJASIRIA MALI HUPEWA KWA UNDANI HAPA TZ BORA UPATE CHETI
 
ni jamb nzuri ila ttzo lni mfumo wa elimu kwa dunia ya sahivi tulipaswa tutilie mkazo soma la ujasiliamali from primary to university ila mfumo wetu wa elimu haupo hivyo na vijan wengi wa tz ni lugha kiingereza kinasumbua sana na hawapendi kujisumbua kufuatilia vitu pia tatizo lingine naloliona ni vijana wengi kurizika mapema kijan wa kibongo ukimpa bodaboda tu aendesh miezi 3 kitambi teyar unategemea huyo atawaza mradi wa mil 100..bado tuna safar ndefu sana labda tubadil sylabus zetu aisee...
 
Mkuu tunaomba utujuze zaidi basi... Maana wengine bado hatujakupata vizuri.
 
Kelele tu, weka link hata 1 tu ya wafadhili wanaotafuta vijana wa Tz! Ulishaangalia hayo masharti? Watu wengine bwana! Wewe umeshatuma ngapi na ukapata ngapi?
 
Mkuu weka link hapa. Mimi nimeshajaribu taasisi kadhaa za hawa wanaotoa Loans au Grants lakini majibu ni negative.

Nitafurahi sana kama ukiweka links hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…