Fursa zinazopatikana maeneo ya migodini

Dali Mpofu

Senior Member
Joined
May 9, 2021
Posts
173
Reaction score
328
Naomba niende chap kwenye point yangu. Nimekuwa mzoefu na sehemu za mgodi kwasababu pia nimefanya kazi mgodini,huko buana kuna fura nyingi ambazo zina ela nzuri tu.

Mfano kwa mtu abaeweza akapata spare za machine za mining, magari na mining equipment machine zote utapata ela sana.

Lakini pia kuna zile PPE kama dustmask, gloves, grass pamoja na zile kofia ngumu. Utapata ela. Nakusihii changamkia hii kitu km unauwezo wa kuzipata.

Halafu pia kama unavyo naweza nikayachukua kwako tukafanya biashara. Huko migodini kuna population kubwa ya watu wanaitaji wale wapate mahitaji ya muhimu zote izo ni fursa. Kuna makampuni wanaitaji watu wa kusambazia vifaa vya kazi mfano makampuni ya usafi,makampuni ya upishi na nk. Tusikariri mjini tuu ndugu zangu kuna fursa ziko porini huku km una mtaji wako umetusua.
 
Ngoja nijiweke sawa nakuja
 
Nje ya mada kidogo Mining sector is booming in kanda ya ziwa wazee kuanzia MWANZA, geita yote, simiyu, kagera hiyo ni balaa nasikia na singida huko wachina kama wotee

Namaanisha kuna wawekezaji wakigeni wengi mnoo sijui ndio mama anafungua nchi au tunaibiwa(waturuki, wachina,wahindi, wasudani kaskazin wale,) ni wamejaa kanda ya ziwa wengine wanakodi apartment zoteee pale town Duuh.

Kama anavosema mwamba hapo tuchangamkie fusra hizo japo sisi ni vibarua tu kwenye mali zetu wenyewe. NARUDIA TENA MINING SECTOR IS BOOMING IN KANDA YA ZIWA.
 
Ntaji shngapi....wengine tuna hela zimelala tu benk na kumeshakucha
Km una ela ni vyema ufike mwenyewe uone lkn sehem za mgodini fursa ni nyingi,watu ni wengi wote wanaitaji kula kwaio hata ukipata kampuni ya upishi unaweza ukawa wakala wa mazao ya chakula. Kwaikifupi mambo ni mengi yenye ela
 
U Uko sahihi, ukienda Sengerema kuna kampuni inafanya expolation na wapo hatua za mwishoni kuna mali nyingi pale.
 
Migodi ni mingi inatemeana wewe utakuwa wp bado kuna mgoni mpya nyanzaga Sengerema ambao utakuwa mgodi wakwnza east africa,maana ina pit 3 ambazo zote ni undergriund kwaio fursa zinaongezeka tusikariri mjini
Nyazaga ya Sengerema?kata ipi mkuu?
 
Migodi ni mingi inatemeana wewe utakuwa wp bado kuna mgoni mpya nyanzaga Sengerema ambao utakuwa mgodi wakwnza east africa,maana ina pit 3 ambazo zote ni undergriund kwaio fursa zinaongezeka tusikariri mjini
Watu wakasome mining kuna ulaji eeeh
 
Ila wakumbushe maisha ya kule sio lele mama.....yani kule ata kama una biashara utaishi kama mkimbizi.

Kwakifupi kama mtoto wa mama,biashara za migodini hutoziweza kule kuna kila aina ya ushenzi na uchafu.

Labda biashara iwe nje kidogo na machimbo.
 
Mgodini kuna starehe sanaaa kwaio wewe na akili zako
 
Unaweza tuambia eneo husika lenye migodi Kwa hapa tz.
Na angalau niingie na mtaji wa shingapi kama nahitaji kuwa katika kutoa huduma muhimu Kwa watu
 
Unaweza tuambia eneo husika lenye migodi Kwa hapa tz.
Na angalau niingie na mtaji wa shingapi kama nahitaji kuwa katika kutoa huduma muhimu Kwa watu
Ambazo nina uzoefu navyo, GGM geita, bully kakola, Northmara mara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…