Futari ipi uipendayo

mh pole, yashankuta hayo skumoja, lakini nkagundua unga ulikua mwepesi mno


Sasa ukafanyaje dia wangu kufanya uzito. Hebu nielekeze viazi vyako ulivifanyaje mpaka ukaweza.
 
Sasa ukafanyaje dia wangu kufanya uzito. Hebu nielekeze viazi vyako ulivifanyaje mpaka ukaweza.

nliongezea unga kiasi kupata uzito, kisha nkaendelea kukaanga baada ya kuhakikisha viazi vyangu vimechovyeka vizuri ngano
 
Asante dia.......nasubiri maelekezo kutoka kwa Mrs Kharusy maana jmosi lazima nipike tena mpaka niweze sikubali


Sorry Kbd, nimechelewa kuiona hii. Viazi vyenye maganda mekundu ndio vizuri kwa katlesi au kachori sababu ni vikavu. vyeupe ni vizuri kwa chipsi hua havinywi mafuta sana. zamani nilikua nateseka nt anymore! tulishawahi kuvichemsha vyeupe vikawa rojo tukaishia kuchanganya na mayai kufanya zege rojorojo badala katlesi...lol
 
Last edited by a moderator:


Asante sana Mrs Kharusy.....sikumbuki nilivinunua vya rangi gani ila baada ya kuvichemsha nikamwaga maji then kwenye sufuria lile na vikiwa vya moto nikaanza kuvisaga kutumia halafu nikaweka ndimu na chumvi......ndo vikakataa kuchomeka maana vilaini mno.

Nitajaribisha tena kesho na nitakupa mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…