Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363

Recipe/Pishi la Raphia Hussein
Mahitaji
- Ndizi Malindi 5
- Nyama ya Ng'ombe½ kilo
- Vitunguu maji 2
- Vitunguu saumu kijiko 1 cha chai
- Nyanya 3
- Binzari ½ kijiko cha chai
- Chumvi kwa kiasi chako
- Hoho 1
- Karoti 2
- Tui la nazi vikombe 2
- Mafuta ya kula kiasi kidogo
Njia
1.shachemsha ndizi kuondoa ubichi mwaga maji weka pembeni.
2.kaanga vitungu maji adi viianza kuwa brown, ongeza vitunguu saumu, kisha nyanya na nyama. acha ichemke maji ya nyanya yakikaribia kukauka weka binzari kidogo ,chumvi,hoho. karoti na ndizi ulizochemsha , koroga na kaanga pamoja ili viungo vishikane na ndizi.
3.Weka tui jingi kiasi acha zichemke hadi ziive vizuri,Epua ndizi jikoni zikiwa na mchuzi (tui) mwingi,zisikauke sana kwani jinsi inavozidi kukaa mchuzi unaganda
4.Mpaka hapo Futari tayari