Huyo mtu muonekano wake tu hana hadhi ya uo mlo...itakua alikua kwenye shindano la makulaji.
Nilipata demu nikiwa kijana kijana, tukatoka kwenda naye Ngwasuma, 2007 hiyo Ngwasuma wanapiga Makumbusho Village
. Ukumbi ulikuwa unajaza sana, Ngwasuma walikuwa wanapendwa sana.
Watu walikuwa wakitoka Tunduma, Mwanza , Kahama etc kuja kuwaona Ngwasuma, hivyo ni lazima uingie ukumbini mapema ukitaak ukae.
Saa 1⅞ jioni niko na huyu binti Ngwasuma, nikaitisha mbuzi portions mbili na yeye chips na robo kuku, nikamwambia agiza nusu kuku akikushinda nitakusaidia.
Mezani nimelaza maji na konyagi kubwa , zamani ilikuwa ya chupa ya round, sio hili jibapa.
Binti aliagiza Coca-Cola nne, ndani ya muda mfupi akawa amezifuta na kaagiza nyingine.
Hadi tunatoka mziki demu kazinywa koka na soda nyingine mchanganyiko zaidi ya 19, kisa hanywi pombe.