"Fyeka Burundi, tusonge mbele" kuna la ziada juu ya kauli hii

"Fyeka Burundi, tusonge mbele" kuna la ziada juu ya kauli hii

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,093
Reaction score
1,899
Tanzania kumekuwa hatufanyi vizuri Kwnye mchezo wa mpira wa miguu kwa muda sasa.
Leo tunashinda, kesho tunapoteza, kesho kutwa tunasubiria mechi ya mwisho na kumsumbua Mungu kwa maombi ili kupata nafasi za kufuzu.

Tatizo kubwa ninaloliona kwa nchi yangu katika mashindano mengi kubwa ni UTIMAMU WA AKILI NA FIKIRA kwa wachezaji. Pili, ni SIASA michezoni.

Tukianza na kauli hii ya "Fyeka Burundi, tusonge mbele " niwapongeze sana waandishi wa habari za michezo, wanania njema sana.
Lakini sambamba na jitihada hizi za wanahabari, je wahusika wakuu "WACHEZAJI" wanaandaliwa vipi kiutimamu wa AKILI zao mchezoni??

Sijapata kufahamu namna ambavyo benchi la ufundi na wataalamu wengine wanawaandaaje wachezaji kisaikolojia? Mazoezi ya viungo na stamina ya mwili sina shida napo, vipi utimamu wa akili ya mchezaji kuelekea mchezo husika.
Je wanajua vizuri majukumu yao?
Je wanajua vizuri umuhimu wa mashindano yenyewe?
Je ni yapi malengo yao?
Je kama mchezaji anafahamu ubora wake au kiwango chake? Nini anatakiwa afanye kuboresha au kubakia na kiwango bora?
Mwisho, Je wanajua athari za mitandao ya kijamii dhidi ya viwango vyao? Wanalewa sifa? Wanaumizwa na maneno mabaya dhidi yao huko mitandaoni? Wanatumia muda mwingi kiasi gani Kwnye mitandao ya kijamii? Kweli wanapumzika wakati wa kupumzika? Au wanapoteza muda mitandaoni?
Haya yote yanachangia utimamu wa akili ya mchezaji.

Waandishi nao, kuliko kusifia kila kitu kuhusu timu yetu na wachezaji wetu, mnafanya uchunguzi wa timu pinzani, yapi mapungufu yao, wanajiandaaje na kipi kifanyike kuwafunga?

Nimeandika huu uzi kwa sababu sifa mnazotoa kwny makala zenu kwa wachezaji wetu saa nyingine zinawalewesha sana kabla ya mchezo na matokeo yake kuichukulia mechi katika uzito usio stahili.
Mfano Mzuri mechi ya Simba SC dhidi ya timu toka Msumbiji. Kila gazeti lilisifia timu ya Simba na wachezaji bila kuangazia wapinzani.
Matokeo yake wachezaji na mashabiki waliaminishwa matokeo bora nyumbani.

Tuache Siasa za michezoni, kusifia bila utaalamu halisi.

Kila la Heri, Taifa Stars.
 
Kiukweli mimi nikiwa kama mdau na mpenda michezo uhususani mpira wa miguu huwa naumia sana kuona taifa langu bado liko nyuma sana kimpira kinyume na ilivyopaswa tuwe.

Taifa letu lina idadi ya watu wa kutosha tu,lina utulivu, maeneo makubwa ya wazi mengi sana na watu wanaoupenda huu mchezo ni wengi mno, lakini tunazidiwa mbali sana na vinchi vidogo vidogo vingi tu hapa Africa ambavyo vina matatizo kibao na havina rasilimali kama tulivyo sisi.

Bila ya kuumiza kichwa kinachotufanya tuwe hapa tulipo ni ukosefu wa maarifa sahihi ya kimichezo, na hili neno maarifa sahihi limebeba vitu vikiwemo maandalizi na miundo mbinu.

Kukosa kwetu maarifa ndio kumefanya tunaenda kwa kusuasua, kwa kubahatisha bahatisha tu.

Leo tukifanya vizuri tunajipongeza na misifa kibao ya kujipaisha hasa media zetu huwa zinajitahidi sana kwenye hili.. Kesho tukiboronga tunakuja na kauli za kinyonge kuwa sisi bado, sjiui hatuwezi, wenzetu wako mbele.. Blah blah blah kibao.

Nikiangalia kwa miaka kumi iliyopita sioni maendeleo yoyote ya maana kwenye soka letu tuliyofanya. Hata ushiriki wetu wa Afcon ulikuwa ni matokdeo ya kuongezeka kwa timu pamoja na group tulilopangwa kwenye hatua ya kufuzu ambalo halikuwa na makali sana.

Tunaenda kucheza na Burundi kwenye kufuzu World Cup Burundi ambayo kwa mtazamo wa haraka haraka ni underdog kwetu. Sijajua mpaka sasa hivi timu yetu Mika kati yake imekaaje sijajua kama wapinzani wetu tumeshaanza kuchunguza madhaifu yao, sijajua hata lini tunaingia kambini na kwa muda gani.
 
Mpira hauhitaji maneno mengi,mpira unachezwa hadharani,ukiujua unaujua tu sio ugenini wala nyumbani na mwisho unahitaji mipango na mikakati katika kufanikiwa
 
Tatzo maneno mengi, kwa mpira waliocheza Burundi afcon sijui km taifa stars atatoboa
 
Tatizo la timu yetu ni kutotabirika. All in all, nawatakia kila la heri.
 
Back
Top Bottom