Gabo: Tupendane tukiwa hai

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
692
Reaction score
880


Msanii wa filamu Ahmed Salim maarufu kama Gabo

Dar es Salaam: Msanii wa filamu nchini Tanzania, Ahmed Salim maarufu Gabo amesema wasanii na wadau wa sanaa wanatakiwa kupendana wakiwa hai.

Gabo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 27, 2019 katika mahojiano na Mwananchi.
Amesema kumekuwa na tabia ya wasanii kuwekeana vikwazo katika utendaji wa kazi jambo linaloweza kuyumbisha tasnia ya filamu.

“Imefikia kipindi hata waliokuwa na mchango hawathaminiki, upendo miongoni mwa wasanii umepotea ndio maana nawaomba tupendane kabla ya kifo kwa sababu huwezi kujua nani atakusaidia na wakati gani, ” amesema Gabo.

Amebainisha kuwa kwa sasa hali imekuwa ngumu katika filamu, kuna uwezekano Mungu akaonyesha kitu endapo watu watashikana kwa kutengeneza kitu kwa umoja.

“Ndugu yangu filamu sasa hivi imekuwa ngumu sana, hatuna upendo wa kuungana mkono, sisi wasanii na wadau tutashindwa kuipeleka tasnia mbele.”

“Tunatakiwa kuamini mchango wa wenzetu waliotutangulia kabla ya umauti kutukuta, tufanye mazuri yao yaliyotufanya sisi kujikita katika filamu,” amesema Gabo.

Amesema umoja, mshikamano, kufikiri kwa pamoja ndio kutaiamsha tena tasnia hiyo badala ya kuwekeana vikwazo.

Chanzo:Mwananchi
 
Suala upendo naona maeneo mengi limeshindikana
 
Wanawake wa bongo movie mbona wao ni bata tu na wanamiliki biashara kubwa tu ki vipi filamu hazilipi? kina uwoya aunt , wema ....nk. wanapeta tu vp kwa wanaume mmekosea wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…