Gabriel Gavu
Member
- Aug 18, 2017
- 10
- 3
MAPINDUZI YA KIFIKRA KWA SASA YANAHITAJIKA
NA ; - GABRIEL GAVU (BSW)
2020
Nianze na kukubali kuwa dunia ni kijiji kwa utandawazi uliopo sasa. Tunahitaji nguvu ya pamoja kuitazama dunia ya leo. Ni dunia hii ambayo naamini hakuna mpaka wa magonjwa na au matukio ila mipaka iliyopo ni ya watu.
Nitaangaza kwenye mambo yafuatayo
Mitazamo ya Katiba
Mitazamo ya watu na masilahi yake
Nguvu ya kundi lililopo madarakani.
Kiongozi Mkuu kupewa madaraka makubwa.
1 - MITAZAMO YA KATIBA
Mitazamo hii imekuwa ya aina mbili Katiba ya Mdomo na katiba ya maadishi. Nchi nyingi zipo kwenye katiba ya maadishi -(written constitutional). Katiba isiyo ya maadishi huwa ina faida kubwa pale nchi inapopata dharula yatukio wakajadiri na wakafikia muafaka kukiridhia kile kilichojadiriwa na mabadiriko yakachukua nafasi.
Hasara yake ni pale ambapo kundi la watu na mitazamo yao likashawishi watu wakubaliane na mabadiriko kwasababu ya nguvu yao na ikafanikiwa kwa sababu tu kundi la mlengo wa kushoto limekosa nguvu na ushawishi. Hapo ndipo pana kupotea na kulingiza taifa kwenye mivutano isiyo ya maana au machafuko ya kisiasa na kiuchumi.
KATIBA YA MAADISHI
Ni utaratibu unaoziendesha nchi kwa muda wote ambao ili ubadiri inakubidi kuendesha mchakato wa katiba. Faida zake ni hizi
Huzuia mabadiriko ya mihemko ya watu wachache na maauzi ya kukurupuka
Hutoa muda wa kutosha watu wachangaie mabadiriko yanayotarajiwa inapohitajika. Hurithiwa na kizazi kinachofuata kupitia maandishi yaliyopo.
Madhaifu yake ni
Inapofikia taifa au taasisi inahitaji kubadiri katiba, mchakato wake hutumia gharama kubwa. Kama kuna makosa ya kimfumo ambayo yanaliingiza Taifa husika kwenye madhara au hasara basi, shida hoyo hudumu sana kusubiri mabadiriko ya katiba
Kundi linalofaidika na utaratibu wa wakati huo kama lina ushawishi mkubwa litaendelea kuitetea hiyo katiba kwa visingizio vingi ilimladi mfumo huo uendelee kufanya kazi.
2-- MITAZAMO YA WATU NA MASILAHI YAKE
Mitazamo haiwezi kufanana na ni moja ya matatizo makubwa kwa sasa ikivurugwa zaid na masilahi ndani ya katiba halali. Fuatilia mifano hii :-
Kumekuwa na wimbi la nchi nyingi kubadiri katiba au kubadiri kifungu ndani ya katiba ili kuwawezesha viongozi waliopo madarakani waendelee kuwepo kwa kuongezewa vipindi vya uongozi. Huu ni mtazamo wa hatari wenye kuvutia masilahi ya kundi lenye kufaidika na mtawala aliyepo madarakani. Kwa nchi za kiafrika hili limekuwa baya zaidi kwa sababu zifuatazo
Mifumo tuliyo nayo siyo rafiki kwa sasa, inamuwezesha kiongozi wa juu kuweka watu wake au watu wa chama chake kwenye ngazi zote za maamuzi. Havyo viongozi wanajikuta kukitambua chama au mtu aliyewateua kuwa ndiye mwajiri wao mkuu, kwasababu hiyo wanakuwa na hofu kuwa kiongozi akibadirika huenda ukawa mwisho wa ajira zao. Kwa maana hiyo hawawezi kutenda haki kwa watu ambao wana msimamo wa kutwaa madaraka. Hili tunaliona kwenye siasa zetu hasa wapinzani wanapokuwa na mawazo mbadara kukosa wa kuwasikiliza.
Vyama vya siasa vina katiba zao nazo hazifuatwi kwasababu ya kuwekwa mitazamo ya watu wa kundi moja. Mfano Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Katiba inaruhusu kiongozi kuongoza vipindi viwili vya miaka mitano hivyo miaka kumi ni ukomo, katikati ya muhura yaani miaka mitano anatakiwa kuomba upya ndani ya chama na wengine pia waombe kugombania nafasi hiyo. Shida inakuja kuonekana kuwa kundi linalomuunga mkono aliyepo madarakani halipo tayari kumpoteza katikati ya muhura na kuishawishi kamati kuu nayo inakubali kuweka vikwazo kwa watia nia wengine wasigombanie nafasi hiyo. Huo ni ukiukwaji mkubwa kikatiba. Mfumo huo hupelekea pia
Kuibua wagombea pekee ngazi zote kutokea baadhi ya maeneo yanayofanya uchaguzi maarufu kupita bila kupingwa. Tanzania Chama cha Democlasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeweza kuliona hilo, wanapokuwa kwenye michakato mbalimbali ya uchakuzi kama utakuwa mgombea pekee lazima upigiwe kura, kama hutafikia asilimia zilizopangwa basi utaikosa nafasi hiyo. Huu ni mfano wa kuigwa.
Kwasababu viongozi wote wenye maamuzi wanakuwa na itikadi za chama tawala basi hata vyombo vya ulizinzi na usalama hujikuta vinawajibika kwenye majukumu ya chama hasa wale wenye nyazifa za maamuzi. Hii hutumika kuhatarisha usalama wa vyama vya upinzani kuonekana ni maadui na kupuuza ushauri wao.
3 - NGUVU YA KUNDI LILILOPO MADARAKANI
Nguvu ya kundi hugeuza mfumo au hushinikiza kuvunja katiba hapa vyombo vya ulinzi vinahusika sana. Mfano: - uchaguzi unafanyika wapinzani wamekubalika wanapewa kura na wananchi viongozi wanaamua kubadiri matokeo kwa namna yoyote ile halafu vyombo vya usalama wamefumba macho. Inapotokea hao wapinzani wanaamua kuchukua hatua wanadhibitiwa na vyombo vya usalama.
Hii ni kwamba vyombo hivyo vipo kiitikadi zaidi. Kwa sasa tuna mfano mzuri wa Malawi ambapo vyombo hivyo vimeonesha kutambua waibu wao na matokeo yake yameonekana kwenye Jeshi la Nchi hiyo, Haki ilitendeka kwe Mahakama zao. Mwisho tunamuona jaji akikataa cheo kwa kutetea mazingira tangulizi. Mabadiriko ya fikra kama haya ndiyo yanatakiwa kwa sasa pongezi kwao na inapaswa kuigwa.
- KIONGOZI MKUU KUPEWA MADARAKA MAKUBWA.
Kuna mitazamo ambayo imekuwa ikfuatwa bila kujiuliza madhara yake. Mataifa mengi tunaona Mwenyekiti wa chama cha siasa ndiye kiongozi mkuu mfano nchi za kifalume Waziri mkuu na nchi zetu Rais wa nchi. Mifumo hii tuitazame kama ifuatavyo
Viongozi hao huwa wanamapungufu kama binadamu wengine, hivyo wakikosea na kuhatrisha usalama wa nchi zao hukosa mtu mwenye nguvu kukemea. Chama kina uwezo wa kumtoa kiongozi madarakani lakini nguvu hiyo hupotea pale kiongozi huyo ni mkuu wa nchi, na ni mwenyekiti wa chama chake kunafanya wajumbe kukosa ujasiri wa kumkabiri mwenyekiti. Hapo wazo langu ni kiongozi wa taifa kama alikuwa mwenyekiti wa chama ajiudhuru wadhifa huo kwa masilahi ya umma.
Mkuu wa nchi kuwa mwamuzi mkuu wa Nyanja zote kwenye uteuzi mashiko yanayohusu masilahi ya taifa hupungua kwa mfano: - Tanzania Rais huwateua Jaji mkuu, Waziri Mkuu, Mkuu wa Majeshi. Hizi ni nyazifa zenye maamuzi ya mwisho juu ya nchi, lakini tunakumbusha hapa kuwa katika ajira utafanya majukumu mengine utakayopangiwa na mwajiri wako.
Mtazamo wangu hapo ningependa majaji wasiteuliwe na Rais au Waziri mkuu bali wateuliwe na chaombo maalumu kama jopo la majaji ili waliahidi hilo jopo nini atalifanyia Taifa, kwa kufanya hivyo hilo jopo litakuwa na uwezo wa kuhoji mapungufu ya jaji mkuu kitaifa. Raisi abaki na wadhifa wa kumuapisha Jaji tu. Mkuu wa Majeshi sina neon naye. Mawaziri wasiwe wabunge ikiwezekana waombe kazi kwenye bunge la nchi husika ili mbunge abaki na mwananchi hapo atatetea kiti chake kwa nguvu kuliko kufikiria uwaziri mpaka kuwasaliti waliomtuma kuwawakilisha.
Kiongozi yeyote aliyeteuliwa na Rais ngazi za mkoa na wilaya huyu asiruhusiwe kuhusika na mchakato wowote wa uchaguzi ili tume iwe huru, kufanya hivyo kutatoa nguvu ya makada wa vyama tawala kujihusisha na siasa za kutetea viti vya wakubwa wao kiajira.
Haya ni machache mwenye mawazo ya kujenga kwa hoja namkaribisha nitajifunza kwake.
GABRIELGAVU – BSW.