Gabriel Zakaria on CCTV

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
LIVE GABRIEL ZAKARIA Mtangazaji wa TBC-1 akiwa LIVE katika Chinese Central Television (CCTV) kuzungumzia masuala ya Ushirikiano wa China na Afrika.

Kwa kweli TBC Jamani wawe makini wanapotuma mtangazaji katika mashirika ya Kimataifa..Gabriel anaweza kufikiri lakini kuweza kupangilia sentensi vizuri ya kiingereza ni tabu sana...


Kijana ni mzuri sana kama mjadala ungekuwa kwa kiswahili.

SIKILIZA HAPA:[video]http://english.cntv.cn/program/dialogue/20120518/107178.shtml[/video]





Today, all eyes are on Africa, the continent once considered the bottom of the world’s economic structure. Six of the ten fastest-growing countries in the world are now in sub-Saharan Africa. Africa is also believed to have the highest rate of return on Foreign Direct Investment (FDI) of any developing region. With this in mind, what is the nature of relations between China and the African continent?
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Dialogue 20120517 China & Africa grow together[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Background Watching:
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Host: Tian Wei

 
na mimi nimeona utafikiri amekaria msumari, mtangaji wa kichina akiwa anamsaadia kwa kusema " i see your point"
 
Aisee nilimuona huyo,kuwasilisha pointi ilikua ishu,hii iwe funzo kwa waandishi wengine,wasome sana vitabu ili waboreshe ngeli zao yaani mwandishi na mtangazaji wa televisheni ya taifa hajui kuelezea point kwa kingereza fasaha ile ni aibu jamani
 
Jamani mbona wazungu wakikosea kiswahili hatushangai.Lakini sisi tunavyokosoana mpaka aibu ungewekwa wewe tuone chako.
 
acha wivu.

Wivu wa nini Kiongozi tunapozungumzia masuala yenye maslahi kwa taifa??

Kijana anatumia Kodi za wananchi kuitangaza TZ kwa staili hiyo, ni vyema tuinapofika kwenye masuala kama haya nyeti TBC wakatuma mtu mwenye uwezo wa masuala ya Kimataifa au biashara za kimataifa kati ya China na Afrika. Sidhani kama hii ilikuwa ni safari tu ya kawaida kwenda kutenmbelea China!!.
 
Jamani mbona wazungu wakikosea kiswahili hatushangai.Lakini sisi tunavyokosoana mpaka aibu ungewekwa wewe tuone chako.
Kiongozi shida sio kiingereza tu, hata kufiukisha ujumbe wenye lugha butu unaweza usieleweke..wachna wenyewe hawajui Kiingereza Vizuri lakini inapofika kwenye masuala yanayohitaji umakini, tujaribu kuwangalia wenzetu, wanapeleka watu makini.

Vituko vya SCC?? Ni pale tunapompa Kaseja apige Penalti ambayo ingetupatia ushindi yeye analeta mzahaa!!
 
mkuu hata mimi nimeona hili tatizo sio kiingereza kibaya tatizo ni point alizotoa kwamba africa tunategeme china na hutuwezi lolote bila china hili tusi kwetu, china wametusaidia kwenye infrastructure its true lakini angalia barabara zilizojengwa hao watu hazina uimara wowote in short china kwa africa ni mzigo tu wametuweka sisi kama dampo la kutupa takataka. huyu jamaa alivyowasifia utazani kweli tunafaidika
 

'kizungu' noma jamani!
 
hajui kjipanga hata kwa kuswahili, jamani kiswahili ni lugha ya kimataifa sasa. jueni hilo
 
Aliniacha hoi pale alipochanganya maneno: 'Africa' na 'African.' Pia 'China' na 'Chinase'. Anyway alijitahidi kidogo.
 
Nilifuatilia kwa makini ule mdahalo Hakka ni aibu tupu Tupu,Jaribuni kufanya mazoezi kuongea kwenye vyombo vya kimataifa..
 
Huyu Kilaza namfahamu, nilishawahi soma nae Advance Certificate ya Radio and TV broadcasting, by the time nikiwa O level, yeye pia alikuwa amemaliza f4m 4 nikaendelea na 4m 5 yeye akaendelea na utangazaji, he was dull since chuo na kujipendekeza kwake kwa wakuu ndio kumemfikisha hapo..
 

Kila jambo lina mwanzo hata Professor huanza na "Assistant Lecture/Tutorial assistant"
 
Kwenye media zetu tuna tatizo kubwa la specialization. Sifa kibwa ya kuwa mtangazaji hapa kwetu ni sauti na muonekano tuu, upstairs haijalishi sana!.

Kwenye TV za wenzetu, watangazaji wa vipindi vya uchumi wamesomea uchumi, watangazaji wa vipindi vya afya wamesomea udaktari, watangazaji wa vipindi vya sanaa ni wasanii, watangazaji wa vipindi vya ulinzi na usalama ni majenerali wastaafu!.

Sisi kwetu mtangazaji ni mtangazaji na atatangaza kila kitu!. Kwa vile tunaingia kwenye digital migration, hakuna jinsi, lazima watangazaji wetu waspecialize vinginevyo no one will watch them with hundred options at a click!.
 

kwa Mtazao wake eti Wachina wameleta maendeleo Afrika kwa Kujenga Viwanja vya Mpira 'akasema "Football grounds" Labda akimaanisha kiwanja kile cha TEMEKE (UWANJA WA TAIFA MPYA). Hakuwa hata na takwimu za kuthibitisha mahala pengine katika Afrika ambapo Wachina wamejenga Uwanja wa mpira wa miguu kama angeulizwa hilo.

Amezungumzia Afrika haiwezi kuishi bila China na kubainisha kuwa "milioni of exports to China from Tanzania especially cotton, sisal, coffee " etc na Kuhoji kwa kiingereza eti "... and if not China, where we could sent our products???> Hajui hata maana ya bishara za kimataifa zinafanyikaji na hakuweza kufahamu ni kiasi gani cha thamani za bidhaa za mazao ya Kilimo ambazo Tanzania imeuza nchini China.

Alipoulizwa kuhusu changamoto za ushirikiana ulipo kati ya Afrika na China alisema "Problem is technology for example machine, how to operate machine is difficult in Africa....." khaaaa..

Mwendesha mada akaingia kati na kumkatiza " oh yes, I get your point...."

Labda TBC waliamua kumtuma yeye kwa kuwa kwa sasa anashikilia lile dawati ambalo Clement Mshana alikuwa akishikilia wakati wa TIDO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…