Gadner G Habash atua EFM

Gadner G Habash atua EFM

Kabewa

Senior Member
Joined
Oct 30, 2009
Posts
136
Reaction score
56
Mtangazaji mahiri Gardner.G. Habash,amejiunga na kituo cha Radio kinachokuja kwa kasi hivi sasa EFM 93.7 cha jijini Dsm ili kuongeza nguvu katika kikosi chao.
Akizungumza leo na waandishi wa habari afisa habari wa EFM Kanky Mwaigomole amesema wameamua kumchukua Gardner kwasababu ni miongoni mwa watangazaji hodari nchini mwenye kipaji cha hali ya juu hivyo kuongeza chachu ya mafanikio katika kituo hicho kipya.
“Gardner ataendesha kipindi kiitwacho Ubaoni kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja kamili jioni kuanzia Jumatatu ya tarehe 03 mwezi wa 11 mwaka huu”alisema Kanky.
Gardner alimaarufu “KAPTENI” alianza kazi na kituo cha Radio Clouds fm na baadaye Times fm ambapo kwa sasa ametua Efm akitanguliwa na wakongwe kama Dj Majey,Dizzo One,Sos B,Denis Ssebo,Maulidi Kitenge,Omari Katanga,Scholastica Mazula na Kanky Mwaigomole.
Asante,
Meneja Uhusiano.
Kanky Mwaigomole.




<a href="http://adserver.adtech.de/adlink/3.0/1332/4452770/0/357/ADTECH;loc=300" target="_blank"><img src="http://adserver.adtech.de/adserv/3.0/1332/4452770/0/357/ADTECH;loc=300" border="0" width="200" height="600" /></a>
 
Hiki kituo kinaomba saiti kwa kasi ya ajabu. Nilisikia mitaani ni cha kigogo mmoja mkubwa nchini.
Wadau kama wanafahamu hili watatuthibitishia ukweli wa hilo
 
Wameajiri mlevi hakuna kitu hapo!Pia atakua amejua hakuna kosa kubwa kama kuishi kwa kumtegemea mwanamke matokeo yake brother man wote hata kibanda cha kuishi hana.
 
Akizungumza leo na waandishi wa habari afisa habari wa EFM Kanky Mwaigomole amesema
Asante,
Meneja Uhusiano.
Kanky Mwaigomole.
Mimi wajameni ni macho tuu na dimples za huyu Kanky!.
MLZ_3528-199x300.jpg
 
Moja ya watu wasiojitambua na wasiojua kipi wanapaswa kufanya kulingana na wao walivyo ni huyu jamaaa
pombe nyingi+utegemezi=?!
Kwa kipaji alichonacho ktk kutangaza angekuwa mbali lkn sasa!
 
Mtangazaji mahiri Gardner.G. Habash,amejiunga na kituo cha Radio kinachokuja kwa kasi hivi sasa EFM 93.7 cha jijini Dsm ili kuongeza nguvu katika kikosi chao.
Meneja Uhusiano.
Kanky Mwaigomole.


Niliwahi kuandika Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!
Wanabodi,

Jee Roho za Waliokufa Zinaweza Kuwaita Walio Hai?.
Jibu ni yes, ndio maana kwa baadhi ya mila, wamama wajawazito hawaruhusiwi kwenda makaburini, ili waliolala wasije wakaviita vichanga, na matokeo yake vikaitika na kupata still born.
Kwenye mahusiano kuna kitu kinaitwa Soul Mates, na hii ndio subject matter ya uzi wangu huu.

Hitimisho.
Kwa vile kwa sisi binadamu wote hapa duniani tuko safari tuu, kuelekea kwenye makao ya milele na maisha ya milele, tusiwalilie waliotangulia na kuhuzunika saana kwa kuwakosa, tuhuzunike kibinaadamu, kwa kulia kwa kiasi tuu, kisha maisha ni lazima yaendelee, bali pia tujiangalie sisi wenyewe, kwa nafsi zetu, jee tumejiandaa kuitika wito wakati siku yetu na saa yetu ikitakapofika?.

Kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa.
RIP Ephraim Kibonde na Ruge Mutahaba na wengine wote waliotangulia, nyinyi mbele sisi tuko nyuma yenu, sote sisi ni wa Kwake na Kwake tutarejea.
Paskali
Marafiki waliotangulia, wanazidi kuitana...

View: https://youtube.com/shorts/KMVmvFPjui4?si=G28gCVGn1VUc-Jbr
nyinyi mbele sisi tuko nyuma yenu, sote sisi ni wa Kwake na Kwake tutarejea.
Rip Gardner G Habash, Kapitain
Paskali
 
Huyo afisa habari wa EFM Kanky Mwaigomole nimejikuta namgugo.
 
Back
Top Bottom