Nipo Tokyo, Japan. Nimeshapazoea. Leo asubuhi tulikuwa na mtetemeko wa ardhi mkubwa kuliko kawaida (6.4) lakini maisha yanaendelea na hamna damage yoyote.
Isingekuwa issue ya demokrasia, ningeishi UAE au Oman. Huko pia ni nyumbani.
Boss, ni vigumu kubadilisha fikra za binadamu. CCM ni ile ile. Viongozi wamebadilisha nguo za Mao na kuvaa suti za Muiingereza kwa shingo upande.
Upinzani ni wale wale. Nch nyingi kiongozi wa upinzani lazima ajiuzulu kama akishindwa katika uchaguzi. Sisi sura ni zile zile. Hamna damu mpya na sitemegei watachukua uongozi miaka ya karibuni. Na hata wakija wepya, CCM inawakaba koo na kuiba kura ili waongoze wao tu.
Mimi nimefunga mikoba yangu na sijaangalia nyuma tena.
I lost hope.