Gaius Julius Caesar, Mwanasiasa pekee aliyewahi kuwa na ushawishi mkubwa Duniani

Gaius Julius Caesar, Mwanasiasa pekee aliyewahi kuwa na ushawishi mkubwa Duniani

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
GAIUS JULIUS CAESAR; MWANASIASA PEKEE ALIYEWAHI KUWA NA USHAWISHI MKUBWA ZAIDI DUNIANI.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Sunday-29/05/2022
Marangu Mtoni, Kilimanjaro Tanzania

Katika historia ya dola 10 kubwa duniani zilizowahi kuitawala dunia yani "World Hegemony" (World Super-Supremacy power), huyu jemedari Gaius Julius Caesar, hushika namba moja kwa umaarufu na ushawishi duniani na pia namba 1 kwa viongozi waliowahi kuwa na nguvu ulimwenguni.

Caesar ni kutoka katika ukoo wa kikabaila (feudalism clan) wa babu yao aliyeitwa Sextus Julius Caesar ambaye ndie babu yake Julius Caesar, Gaius Julius Caesar ni mtoto wa Aurelia, na Kabaila Gaius Celius Caesar, moja ya familia maarufu Rome na senator wa Roman Senatus.

Gaius Julius Caesar katika maisha yake rasmi alikuwa na mtoto mmoja aliyeitwa Julia, mwingine ni Caesarion aliyezaa na Kleopatra japo huyu akutambulika sana.

Mtoto mwingine ni mpwa wake aliye muasili (adoptive) aliyeitwa Augustus, huyu Augustus ndio hufahamika kama "The Roman Principate" au pia hufahamika kama "Pax Romana".

Huyo Augustus ndio Oktaviano yani Augustus of Prima Porta, mtawala (emperor) wa kwanza wa Roma aliyetawazwa na kutawala kuanzia
16 January 27 BC mpaka tarehe 19 August AD 14.

Caesar ndio alama ya watawala wenye ushawishi na nguvu ulimwenguni, jina lake limeacha kumbukumbu kubwa duniani, utakapowataja Alexander the great, Menes, Charlemagne (Kololo Mkuu), Æthelstan the great, Louis the German, Cecrops, Rurik of Ladoga. Ghensi Khan, Jimmu, Qin Shi Huang the great, Sargon of Akkad, Cyrus the Great na Osman Ghazi, huwezi kuliacha jina la Caesar ambalo litachorwa kwa wino mwekundu.

Caesar alikuwa mtu na nusu, jemedari mkuu na mpambanaji asiosaulika duniani.

Yes, namanisha Gaius Julius Celius Sextus Caesar, mwasisi wa Dola-Himaya ya Rumi (Rome Empire), huyu Gaius Julius Caesar au Kaisari kwa wengi wanavyomjua alikuwa jemedari aliyeacha alama kubwa ulimwenguni mpaka sasa.

Kwanza kabisa yeye ndio Mwanadamu wa kwanza sura yake kuwekwa kwenye pesa, kabla ya hapo hakuna sura ya kiongozi yoyote yule aliyewahi kuwekwa kwenye sarafu ya pesa.

Pili, yeye ndio Mwanadamu wa kwanza kabisa baada ya kifo chake aligeuzwa kama mungu wa dola, baada ya yeye kufariki huko Rome Empire, walianza kumuabudu kama Mungu, Binadamu mwingine aliyepewa hadhi hiyo ni Mfalme wa kwanza wa Japan aliyeitwa Jimmu.

Tatu, Gaius Julius Caesar ndio Mwanadamu wa kwanza duniani jina lake kutumika kama cheo rasmi cha ukuu wa Dola, neno "Kaiser" lilitumika ulaya yote kurejelea cheo cha mfalme.

Nne, Gaius Julius Caesar ndio Mwanadamu wa tatu duniani kutembea umbali mrefu kwa faransi akiwa nyuma ya mfalme Timul (Ghensi Khan) na Simón Bolívar.

Tano, Caesar ndio Mwanadamu wa pili kupigana vita vingi duniani.

Pamoja na mengine mengi Gaius Julius Caesar aliacha alama kubwa kwenye historia ya ulimwengu kama walivyo acha waasisi wa Ulaya akiwemo mfalme wa kwanza wa Ufaransa Charlemagne (Kololo Mkuu), mfalme wa kwanza wa Uingereza Æthelstan the great, Mfalme wa kwanza wa Ujerumani Louis the German, Pia mfalme wa kwanza wa Ugiriki Cecrops na Alexander the great na mfalme wa kwanza wa Russia aliyeitwa Rurik of Ladoga.

Siku nyingine ntakuja kueleza historia za hao mabwana 5 ambao ndio mababu wa Ulaya, bara liloendelea kuliko mabala yote duniani, bara ambalo limestaarabika na ndio bara pekee linalovutia maendeleo kwakua ndio bala la kwanza kupokea maendeleo ya kibinadamu ulimwenguni.

Ila kwa leo, Tutamuangazia mwasisi wa Dola-Himaya ya Rumi au Rome Empire, wengine huita Miliki ya Rumi au Dola takatifu ya Rome ambayo mwasisi wake ni Gaius Julius Caesar au Kaisari.

Caesar the prima Roman.....

Huyu Caesar alikuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi wa Roma ya Kale, alikuwa jemedari mkuu wa ile iliyokuwa Jamuhuri ya Roma, anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayo onekana kuathiri dunia hadi leo.

Alikuwa kiongozi wa kijeshi aliye iteka Gallia (leo inayoitwa Ufaransa) na kuifanya jimbo la dola ya Roma, Gallia ilitawaliwa na Rome kwa zaidi ya miaka 300 na Kutokana na hilo, lugha ya Kifaransa ina ukaribu sana na Kilatini ambayo ndio lugha ya Roma ya Kale.

Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kumtangulia, akatangazwa kuwa Mungu, Jina lake liliidhinishwa kuwa jina kwa ajili ya cheo cha watawala wa Kiroma waliomfuata.

Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama,vile Kijerumani ("Kaiser"), Kirusi ("Tsar") na Kiswahili ("Kaisari" kutokana na neno la Kijerumani).

Huyu Caesar wakati wa utawala wake aliunda kalenda ambayo imekuwa msingi wa kalenda ya kimataifa leo (Kalenda ya Juliasi), Kwa heshima yake, mwezi wa saba unaitwa Julai kurejelea heshima ya jina lake "Julius".

Ni yeye Caesar aliyeweka misingi iliyoifanya Dola la Roma kuja kuitawala dunia kwa miaka 1200 ya moja kwa moja na miaka mingi hadi sasa isiyo ya moja kwa moja.

Gaius Julius Caesar alizaliwa Rome, kutoka katika familia ya makabaila wenye nafasi kwenye bunge la Roma liloitwa Senatus, yeye aliingia katika siasa akiwa na miaka 19, akachaguliwa kwa vyeo mbalimbali kwa vipindi vya kawaida wa miezi kadhaa hadi mwaka moja.

Baadae cheo chake muhimu cha kwanza kilikuwa ni mkuu wa koloni la Kiroma la Hispania, alifaulu kushinda ghasia ya Wahispania wenyeji waliojaribu kuwafukuza Waroma kutoka uhispania.

Caesar aliporudi Roma alitajirika na kujipatia sifa kama kiongozi wa kijeshi pia mwanasiasa aliyeliokoa koloni la Kihispania lisitoke mikononi mwa Rome.

Julius Caesar na triumviratus......

Caesar aliitaji nguvu zaidi, alitaji kutanua himaya na ushawishi zaidi, hivyo akatafuta umoja na watu wenye ushawishi, hivyo Caesar akajiunga na wanasiasa wawili walio kuwa na ushawishi jijini Rome.

Ambao ni Gnaeus Pompeius Magnus, aliyekuwa mkuu wa wanajeshi na Marcus Licinius Crassus, aliyekuwa tajiri mkubwa kushinda Waroma wote kipindi hicho, siunajua ukitaka kuwa na mamlaka lazima ukamate sehemu mbili, pesa na jeshi yani nguvu.

Hivyo wote watatu waliunda umoja ulioitwa "triumviratus", yaani utatu mtakatifu, umoja huu wa wanaume watatu ukawa ndio habari ya mjini huko Rome na pande zote za dunia kipindi hicho, wakashika mamlaka katika dola.

Caesar alichaguliwa kwa cheo kikuu cha mtawala yaani Consul, kwa mwaka 59 KK, Baada ya mwisho wa kipindi chake kuisha alijipatia cheo kingine cha Proconsul au gavana wa eneo la Gallia (Italia ya Kaskazini na eneo dogo la Ufaransa ya Kusini).

Alitumia nafasi hii kuanzisha vita dhidi ya makabila ya Gallia, yaani eneo lote la Ufaransa, Uswisi na Ubelgiji ya leo.

Katika miaka minane ya utawala wake yani toka mwaka 58 - 51 KK alitwaa Gallia yote, kisha akaiingia nchini Ujerumani na
kuvuka bahari akashambulia upande wa kusini akielekea Uingereza.

Caesar mwenyewe aliandika kitabu cha "De bello gallico" (yaani Vita ya Gallia) alichoelezea mapigano yake, Kitabu hicho kina habari muhimu za kihistoria juu ya utamaduni wa makabila ya Gallia, Ujerumani na Uingereza aliyopigana nayo.

Baada ya kufanikiwa huko Gallia na kujenga jeshi kubwa tena hodari, jeshi ambalo liliogopwa ulaya yote, utawala wake ulienea ulaya yote ya magharibi.

Nchi zote za Ujerumani, Ufaransa, Hispania, Uingereza, Uberigiji, uholanzi zikawa chini ya Julius Caesar, kufatia jeshi lake kuwa lenye nguvu wanasiasa wengine huko Roma walianza kumwogopa wakajaribu kumzuia asirudi Italia.

Mwenzake Crassus kutoka kwenye ile "triumviratus" alikuwa amekufa tayari vitani Mashariki mwa dola ya Roma, mwenzake Pompeius alimwogopa Caesar akajaribu kuwashawishi viongozi wengine kumsimamisha.

Lakini mwaka 49 KK Caesar aliongoza wanajeshi wake warudi Italia, Pompeius na wapinzani wake kusikia ujio wa Caesar wakakimbia Roma wakaenda Ugiriki lililokuwa jimbo la dola ya Roma, ile triumviratus yao ikawa imekufa, urafiki ikiingia tamaa na ubinafsi hauwezi kuendelea, ndio wahenga husema.

Mwaka 48 KK, Caesar akachaguliwa tena kuwa Konsul, akamfuata Pompeius na jeshi lake huko Ugiriki akamshinda katika mapigano.

Pompeius kuona ameshindwa vita akaamua kukimbia Ugiriki na
kwenda Misri lakini mfalme Ptolemaio XIII wa Misri alimwogopa Caesar akamua Pompeius akampatia Caesar kichwa chake alipofika Misri.

Caesar alikutana na dada yake Ptolemaio, aliyeitawa Kleopatra akampenda na kuzaa naye mtoto mmoja, kisha akamsaidia Kleopatra kuwa malikia na mtawala wa Misri.

Caesar alirudi Roma kutoka Misri akiwa mshindi dhidi ya wapinzani wote, Bunge la Senatus lilimpa cheo na madaraka ya dikteta (Dictatorius) kwa miaka 10.

Baada ya ushindi mwingine dhidi ya wapinzani huko Hispania bunge lilibadilisha azimio hilo na kumpa cheo cha dikteta wa maisha, Caesar alipokea azimio hili.

Baadhi ya wabunge waliogopa kwamba nia yake ilikuwa kuja kuwa mfalme wa Roma jambo lililokuwa marufuku katika jamhuri ya Roma.

Kikundi cha wabunge makabaila wa familia za kale kiliunga mkono mpango wa kumuua Caesar, wakaandaa mpango wa kumuua na hatimae wakamua Caesar bungeni tarehe 15 Machi 44 KK kwa kumdunga kisu mara 23.

Julius Caesar aliuawa kwa kuchomwa kisu na kundi la maseneta wa Kirumi, akiwemo Gaius Cassius Longinus, Marcus Junius Brutus na Publius Servilius Casca Longus.

Mauaji hayo yalifanyika mnamo Machi 15, kwenye bunge la Senatus lililokuwa likifanyika kwenye ukumbi wa michezo wa Pompey.

Wakati anauwawa Caesar anasemekana alimtambua mpwa wake Brutus akamuliza kwa maneno yake ya mwisho "Hata wewe mwanangu?", Siku zote kikulacho kipo karibu yako.

Mpango wa kumuua Caesar....

Julius Caesar alikuwa na maadui wengi katika Seneti ya Roma ambao walihofia nguvu na ushawishi wa Caesar katika utawala wake.

Wakapanga njama za kumuua, walijadili mbinu tatu za kumuua Caesar, mbinu yao ya akwanza ilikuwa ni mpango wa uchaguzi ili kumuondoa madarakani, mpango huu wakaona utashindwa kutokana na nguvu ya Caesar.

mpango wa pili ilikuwa ni wa sumu nao wakaona utashindwa, hivyo wakaandaa mpango wa kumuua kwa kumchoma visu.

Wala njama ya mauaji walichagua siku ya Machi 15, iliyoitwa "Ides de March", iwe ndio tarehe ya kumuua Caesar.

Siku hiyo ilikuwa sawa na Siku ya Mwaka Mpya na Siku ya Ushuru, huko Rome, siku ya Ides of March pia ilikuwa siku ambayo Warumi walisherehekea Mungu wa Kirumi Jupiter na mungu wa kike wa Kirumi Anna Perenna.

Hivyo itoshe kusema kwa siku hiyo ilikuwa siku muhimu sana ambayo Seneti ya Roma ilifanya mkutano wake muhimu zaidi.

Wala njama ya mauaji walichagua ukumbi wa michezo wa Pompey ili kumuua Caesar.

Siku ya kuuwawa kwake Caesar alionywa na mtabiri wake kuwa kitu kibaya kingemtokea lakini Caesar mwenyewe alipuuza hilo.

Caesar kabla ya kifo chake alikuwa amemteua mpwa wake Oktaviano kuwa ndio mrithi wake iwapo atafariki vitani, ikumbukwe kuwa huyu Oktaviano ndie aliyekuja kujulikana baadaye kama Caesar Augusto na ndie alikuja kuwa mtawala wa kwanza wa Dola ya Roma.

Huyu Augusto ndie aliyevunja Jamuhuri ya Roma na kuanzisha rasmi Dola ya Roma na kuanza kutumia falsafa ya Julius Caesar katika utawala wake, Augusto anahesabika kama mtawala wa kwanza wa miliki ya Dola ya Roma kwasababu ndio Mfalme wa kwanza wa Rome Empire aliyefuata baada ya kuivunja Jamuhuri ya Roma iliyokuwa chini ya Bunge la Senatus.

Baada ya Caesar Augusto kuchukua madaraka alilipiza kisasi kifo cha Julius Caesar katika kipindi cha vita ya wenyewe kwa wenyewe na kuua wapinzani wote wa Caesar.

Miaka miwili baada ya kifo cha Julius Caesar bunge la Senatus lilimtangaza Gaius Julius Caesar kuwa Mungu.

Pia ikatangazwa tarehe 15 March kama siku maalumu ya kumbukumbu yake inayorejelea tarehe ya 15 kama "Ides of March", kama siku muhimu huko Rome kukumbuka siku Julius Caesar alipo uwawa.

Baada ya kifo cha Julius Caesar Jamuhuri ya Roma ilivunjika na kuzaliwa miliki ya Dola ya Roma ambayo ndio iliyokuja kuwa miliki kubwa na himaya iliyodumu kwa muda mrefu ikiitawala dunia.

Misingi ya Dola ya Roma ilianzishwa na Julius Caesar na kuendelezwa na Augusto Caesar ambae mwezi wa nane (August) umeitwa kwa jina lake.

Dola ya Roma ilikuwa milki kubwa ililoenea kwa karne kadhaa katika nchi zote zinazopakana na bahari ya Mediteranea na maeneo mengine duniani.

Karenda ya Julian (kirumi) inayotumika sasa ilianzishwa na Julius Caesar, masaa tunayotumia sasa yalianzishwa na Julius Caesar.

Hivyo "CAESAR" anabakia kuwa alama muhimu Ulaya na duniani.

Kuna msemo usemao "Katika maisha hata marafiki zako kuna kipimo cha mafanikio wamekuwekea, Ukivuka tu kipimo hicho tambua hao marafiki zako watakuchukia", ndicho kilichomtokea Caesar.

Alivuma, marafiki wakamchukia, kisha wakamuua hata ndugu zake walishiliki kifo chake.

Caesar aliwahi kusema "If you must break the law, do it to seize power: in all other cases observe it."

-Julius Caesar

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu

Written by Comred Mbwana Allyamtu
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

FB_IMG_1653819320239.jpg
 
Ili jenerali uwe na nguvu unahitaji makamanda wa nguvu Julius Caesar alikuwa na makamanda wake Kama Mike Antonio au Mike Anthony, Ceasario, Pombeo japo badae walitofautiana Gayas Julius Caesar alikuwa na kikos hatari kiliitwa Thirteen hata hyo Cyrus The great wa Persia alikuwa na makamanda WA kaz Role model wa Caesar alikuwa Alexander the great Julius Caesar alitaka awe Kama Alexander
 
Sahihi kabisa, Caesar alipofika Ugiriki alitembelea kaburi la Alexander the great na kunena maneno haya "Natamani ningekuona ukiwa hai, napita njia zako"
 
Ili jenerali uwe na nguvu unahitaji makamanda wa nguvu Julius Caesar alikuwa na makamanda wake Kama Mike Antonio au Mike Anthony, Ceasario, Pombeo japo badae walitofautiana Gayas Julius Caesar alikuwa na kikos hatari kiliitwa Thirteen hata hyo Cyrus The great wa Persia alikuwa na makamanda WA kaz Role model wa Caesar alikuwa Alexander the great Julius Caesar alitaka awe Kama Alexander
Sahihi kabisa, Caesar alipofika Ugiriki alitembelea kaburi la Alexander the great na kunena maneno haya "Natamani ningekuona ukiwa hai, napita njia zako"
 
Back
Top Bottom