Gamba la Kobe lina mchango wowote katika utagaji wa kuku?

Mabobish

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
367
Reaction score
282
Wadau naomba kupata uzoefu kwa Wafugaji wa Kuku juu ya matumizi ya gamba la Kobe katika kukuza utagaji wa mayai kwa kuku. Nimenyetishwa kwamba ukitaka kuku watage mayai na kuzaliana kama wendawazimu ni kutumia Gamba la Kobe katika kuwanyweshea maji.

Naomba ku-share ujuzi na uzoefu kwa yeyote mwenye uzoefu na ujuzi wa jambo hili kwani mie ni mfugaji wa kuku wa kienyeji na ambition yangu ni kuongeza idadi ya kuku na kufuga kibiashara.

Mapovu hapana tushee uzoefu na kujengana kiuchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ukiweka meno ya tembo kama hukufuata kanuni bora za ufugaji kama;
1. Banda bora
2. Mbegu bora ya kuku
3. Chakula bora
4. Ufuatiliaji wa Chanjo na kutibu magonjwa
5. Uwiano sahihi wa mitetea na majogoo (10:1)
6. Utunzaji bora wa mayai na vifaranga.
Hakika usipo fanya hayo hilo gamba la kobe halitasaidia lolote.
 


Hayo mambo ya kizungu, sisi tunataka mambo ya kiafrika, vipi gamba la kobe linaweza kuuongeza productivity ya kuku??!!
 
Hayo mambo ya kizungu, sisi tunataka mambo ya kiafrika, vipi gamba la kobe linaweza kuuongeza productivity ya kuku??!!
Hebu acha ushirikina ndugu mambo ya kizungu kivipi wakati hizo nilizotaja hapo juu ni kanuni za ufugaji bora.

Ila kama unataka kufuga kishirikina na kimazindiko kutumia gamba la kobe kama chombo cha kuwekea maji nadhani haitosaidia ungetafuta hirizi uwafunge hao kuku pia kuwa chanja chale.
 


Hivi ushirikina unaujua au unaongea tu?!!, ushirikina ni nini???-- tuanzie hapo kwanza.
 
Ilitakiwa kwa anaejua kama aje kumjibu kama ni kweli au si kweli, then ndio muanze kumshauri hayo mengine

Kwanza ameshaanza kwa kusema no mapovu kubuni swali lake, then ndio mumpe hayo maelekezo mengine

phat_07
 
Jibu lake ni NDIO kwa enzi hizo kwa sasa wape lishe bora usisahau kuwapa na chokaa kwa sababu ndiyo walikuwa wanaipata kwenye hayo magamba ya kobe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…