LGE2024 Gambo aonya wenyeviti wa Serikali za mitaa kutumia mihuri ya serikali kujinufaisha

LGE2024 Gambo aonya wenyeviti wa Serikali za mitaa kutumia mihuri ya serikali kujinufaisha

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Mashaka Gambo, ameongoza wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo lake, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na utumishi wa kweli kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kampeni hizo, Gambo amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa watakaoshinda katika uchaguzi huo kutekeleza majukumu yao kwa uwazi na uadilifu, badala ya kujinufaisha kupitia mihuri ya serikali.

Mbunge huyo ameeleza kuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa hana mishahara rasmi bali anapata posho, hivyo ni muhimu kwa wagombea kuelewa kuwa nafasi hiyo si ya kutafuta maslahi binafsi.

Soma Pia:
Gambo amesisitiza wenyeviti wa serikali za mitaa kuwa kipaumbele chao kiwe kuwasemea, kusikiliza, na kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yao. Ameeleza kuwa kazi ya mwenyekiti ni kuongoza na kuwakilisha maslahi ya wananchi, badala ya kujihusisha na siasa za maslahi binafsi.

Aidha, Gambo ametoa wito kwa wenyeviti hao kuhakikisha kuwa vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu katika mitaa yao wananufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri ya Jiji la Arusha.

 
Back
Top Bottom