Pre GE2025 Gambo na Kawaida waongoza Parade ya Mamia ya Bodaboda kuelekea mkutano wao wa mwaka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Leo, Desemba 27 Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, akiambatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) nchini Tanzania, Mohammed Kawaida, wamewaongoza mamia ya vijana wa Mkoa wa Arusha wanaofanya kazi ya usafirishaji wa abiria kwa pikipiki (bodaboda) kuelekea Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC, jijini Arusha.
IMG_2062.jpeg

Msafara huo wa kipekee ulikuwa sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa mwaka. Mkutano huo ulilenga kutoa elimu ya ushirika, elimu ya mikopo, pamoja na kuzindua mfumo wa kidigitali kwa ajili ya utambuzi na uendeshaji bora wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya bodaboda.
IMG_2064.jpeg

Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Mohammed Kawaida, ambaye aliwasisitiza vijana kuhusu umuhimu wa kutumia teknolojia na ushirika katika kuimarisha uchumi wao na kuboresha huduma zao kwa wateja.
IMG_2063.jpeg
 
Sasa kama ni mkutano mkuu wa bodaboda ingefaa watembee kwenye agenda za mkutano sasa hii mara mitano tena inatoka wap?
 
Leo, Desemba 27 Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, akiambatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) nchini Tanzania, Mohammed Kawaida, wamewaongoza mamia ya vijana wa Mkoa wa Arusha wanaofanya kazi ya usafirishaji wa abiria kwa pikipiki (bodaboda) kuelekea Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC, jijini Arusha.
View attachment 3186436
Msafara huo wa kipekee ulikuwa sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa mwaka. Mkutano huo ulilenga kutoa elimu ya ushirika, elimu ya mikopo, pamoja na kuzindua mfumo wa kidigitali kwa ajili ya utambuzi na uendeshaji bora wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya bodaboda.
View attachment 3186437
Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Mohammed Kawaida, ambaye aliwasisitiza vijana kuhusu umuhimu wa kutumia teknolojia na ushirika katika kuimarisha uchumi wao na kuboresha huduma zao kwa wateja.View attachment 3186438
Kipindi cha bodaboda kupiga pesa
 
Back
Top Bottom