View attachment 3626888
Sahau kabisa muundo wa Zamani (Menu ya Zamani), toleo jipya la FC 27 The Grounds ndiyo moja ya mabadiliko makubwa yanayotarajiwa kuja kwenye EA Sports FC 27.
Badala ya kuchagua mechi kupitia menu za kawaida, mchezo umebadlika unakupeleka kwenye dunia ya wazi (open world) ambapo wachezaji hukutana, huzunguka na kushiriki shughuli mbalimbali za mpira mitaani.
View attachment 3626889
EA imesajili rasmi jina mode hiyo itaweza kuitwa "FC The Grounds", jambo linaloonyesha kuwa ni sehemu mpya ya mchezo, ingawa maelezo yote rasmi ya gameplay bado hayajatolewa.
๐ข Kinachotarajiwa kwenye The Grounds ni:
โฝ Kutembea kwenye maeneo mbalimbali kwa kutumia avatar yako.
๐ฅ Kukutana na wachezaji wengine mtandaoni.
๐ฅ
Kucheza mini-games, street football na mechi za haraka.
View attachment 3626894
๐ฝ Kubadilisha mavazi, viatu na mwonekano wa avatar.
View attachment 3626895
๐ Kujiunga na mechi kupitia viwanja vilivyopo ndani ya open world badala ya menu za kawaida.
Ni kama ilivyo NBA 2K City ambapo kuna mji mkubwa wa mtandaoni unaoweza kuuzunguka na kushiriki shughuli mbalimbali. Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wana wasiwasi kuwa linaweza kuharibu uhalisia wa Game ๐ฎ.