Makocha wa Yanga na Simba, Miguel Gamondi na Fadlu Davids wakisalimiana baada ya kukutana kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa kuzungumza na waandishi wa habari kuekea mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii.
Simba na Yanga zitamenyana kesho Agosti 8, 2024 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.
Mshindi wa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Simba atacheza na Azam/Coastal Union ambao wanacheza nusu fainali ya pili Zanzibar kwenye Uwanja wa New Amaan kesho.
Msimu uliopita Simba ilitwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Yanga katika fainali kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa suluhu.