Gamondi hadi muda huu kwenye Ardhi ya Tanzania anafanya nini?

Gamondi hadi muda huu kwenye Ardhi ya Tanzania anafanya nini?

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
KUHUSU GAMONDI

Nilidhani baada ya mechi huyu mtu hakupaswa hata kukanyaga Avic town,lakini Kwa mshangao nimeshangaa hadi muda huu yupo tu anadunda kama kitenesi!

Viongozi wa Yanga mnatukosea sana mashabiki na wanachama hadi muda huu!,niwaulize nyie viongozi,Je,huyo Gamondi ni mwanahisa hapo Jangwani kiasi kwamba hafukuziki?

Sitarajii na sitegemei kuona Gamondi akimaliza saa 24 zijazo,mkiendelea kumng'ang'ania huyo kichwa kigumu nitavunja kadi yangu ya Uanachama na nitachoma jezi zote za Yanga na sitonunua tena jezi na sitalipia kadi tena!

KUHUSU UWANJA WA CHAMAZI

Binafsi huu uwanja hauna tatizo,nawashangaa sana mashabiki hoya hoya ambao Wana viherehere na vidomodomo ya kwamba eti, timu iachane na uwanja wa Azam kwasababu ya Hujuma!

Hujuma zipi?yaani timu ifanye vibaya tuseme Hujuma?,hizo hujuma zilikuwa wapi wakati tunacheza na Vital O?,Hizo hujuma hazikuwepo wakati tunashinda mechi nyingine?

Ndiyo yawezekana Kuna wafanyakazi wa Uwanja (Stewards) ambao si waaminifu Kwa kutengeneza mazingira ya kuidhoofisha Yanga na kuwafanya wapinzani wetu watukejeli!

Hebu nielezeni,timu ikiacha kutumia Uwanja wa Azam (CHAMAZI) watatumia uwanja gani?,Kwani hatuelewi uwanja wa Taifa upo kwenye ukarabati?,kwani hatujui uwanja wa New Amani Complex nao wameufunga Kwa muda usiojulikana pia upo kwenye ukarabati?,hebu niambieni tutaenda kuchezea wapi?

Wapuuzi wengine nimewasikia wanasema eti timu ikacheze uwanja wa Mwanza (CCM kirumba) kama uwanja wake wa nyumbani!,hivi huo uwanja mnaujua lakini au mnauonaga kwenye TV mnadhani ni kiwanja Bora? Au mnataka timu iende uwanja wa KMC ambalo Makolo tayari wamesimika mizimu Yao?

Binafsi uwanja kwangu hauna tatizo!

KUHUSU MASHABIKI

Kama Kuna mashabiki nchi hii ambao naweza kusema ni wapuuzi,bila shaka watakuwa mashabiki wa Yanga!

Jana Kuna mwingine kidogo nimpigie hadi niue kwasababu ya ujinga wake,Mimi nipo sehemu tunazungumzia mpira,yeye na kiherehere Chake akataka kuniletea Ujuaji!

Hivi unawezaje ukiwa kama shabiki wa Yanga huna Jezi ya Timu yako?,Hivi unawezaje ukiwa kama shabiki wa timu yako uwanjani uendi?

Timu imechukua Ubingwa mara 3 mfululizo lakini mashabiki wa kuchajaza tu pale CHAMAZI niwa kuwatafuta Kwa tochi,Je mnataka Yanga ifanye kitu gani ili muweze kwenda uwanjani?

Binafsi nawapongeza mashabiki wa Makolo,japokuwa Makolo wanefanya vibaya miaka 3 lakini wameendelea kujaza uwanja wowote pale timu Yao inapo cheza!,Hebu fikiria wangekuwa wanafanya vizuri hali ingekuwaje!

Huku kwetu unakuta shabiki yupo kibanda umiza huko anapiga kelele tu!

Ni lini mtabadilika nyie?

Yangu ni hayo tu jioni ya leo?

N.B - Matusi kwangu ni utuli,tukana sana ili nami niendelee kunukia sana!
 
Anapiga picha
IMG-20241108-WA0006.jpg
 
Mahudhurio vyura:


pesa za kununua wastaafu: Nipooo
Pesa za kesi kutapeli wachezaji: Nipoo
Pesa za fidia mahakamani: Nipoo
Pesa za jezi mashabiki: Hayupooooo
Pesa za viingilio uwanjani: Hayupooo
Pesa za kulipiwa viingilio: Nipoooo, juzi, jana, leo.
Pesa za Supu: Nipooo
Pesa za kumlipa Manara: Nipooo
Pesa za shooting mobeto/Aziz: Nipooo
Pesa za Sindano: Nipooo
Bahasha: Nimejaa tele.
Pesa marefa: Nipooo
 
Tulia wewe acha kelele zako sisi tunataka magoli sio kitu kingine chochote
 
Back
Top Bottom