Gamondi na Benchi lake la ufundi wanapaswa kumvumilia Denis Nkane Kama wanavyomvumilia Clement Mzinze

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Denis Nkane ni Moja Kati ya Talanta kuntu sana katika taifa letu, Talanta hii kocha wa mpira Mohammed Nabi aliiamini kabisa na iliipa matokeo "what a supersub" Naam hakuna asiyekua umuhimu wa wa bwana mdogo Denis Nkane katika kikosi Cha Yanga Sc kipindi Cha Nabi.

Toka amekuja Kocha Gamond bwana mdogo hapati namba kabisa lakini siyo Kwamba Hana kiwango (kiwango kimeshuka) hapana waliopo mazoezini bwana mdogo anakiwasha vizuri Ila tatizo lipo kwa kocha Gamond kumpanga bwana mdogo Denis Nkane.

Nimekua nikijiuliza tatizo ni nin mpaka asipagwe urefu au nini? Na kama ni urefu mbona Nabi alimtumia na ufupi wake?!

Ombi langu kwa benchi la ufundi: Denis Nkane na yeye apewe namba acheze kwani kukaa benchi kila siku bila ya match fitness kiwango chake kinazidi kudumaa.

Kama benchi la ufundi liliweza kumvumilia Guedejr, Jonas Mkude na Clement Mzinze tuliokuwa tunawakejeli na kuwatukana kwa kiwango kibovu nikieepo na Mimi mwenyewe Sasa kwa Nini Denis Nkane asipewe Mechi?!
 
Kila kocha ana mfumo wake. Nabi alikua anatumia mawinga ikawa rahisi nkane kucheza ingawa alikua mchezaji wa rotation, Gamondi anatumia viungo washambuliaji tupu mara chache sana anabadilika kutumia winga pale anapotaka kutanua ukuta wa mpinzani hata farid mussa anacheza mara chache sana yanga ya gamondi
 
Unataka acheze Denis nkane amuweke bench nani
 
Nkane hana jipya aende Mashujaa huko.
 
Nkane alipewa nafasi akashindwa ku perform kombe la mapinduzi .
 
Kila kocha ana mfumo wake. Nabi alikua anatumia mawinga ikawa rahisi nkane kucheza ingawa alikua mchezaji wa rotation, Gamondi anatumia viungo washambuliaji tupu mara chache sana anabadilika kutumia winga pale anapotaka kutanua ukuta wa mpinzani hata farid mussa anacheza mara chache sana yanga ya gamondi
Uko sahihi kabisa. Mfumo wa Gamondi siyo rafiki kabisa kwa viungo washambuliaji aina ya Denis Nkane. Na ndiyo maana hata Jesus Moloko aliondolewa msimu uliopita, ni kwa sababu hakuendana na mfumo wa mwalimu mpya.

I wish wangemtoa kwa mkopo, au kocha angembadilishia majukumu. Ila kiukweli anastahili kufikiriwa walau mara moj moja. Ingawa na ushindani wa namba kwa sasa pale Yanga siyo wa kitoto.
 
Nkane sio mchezaji mbaya na yupo katika umri wa kuendelea kujifunza lakini binafsi sioni kama ana potential ya kuja kuwa na maajabu kivile, aendelee tu kujifunza proffesionalism pale jangwani muda ukifika apewe thank you.
 
Ndio maana nikasema idadi, hapo umenitajia mechi moja wakati Nabi alikaa misimu miwili na Yanga
Hizo ni shida zako, hakuna kocha anayejaribu mchezaji kwenye mechi ya fainali.

Sijui huwa mnatumia kiungo gani kufikiri?
 
Kama alionekana anafaa na ana fit basi Nabi angemjumuisha kwenye first eleven yake au hata kwenye sub. Lakini Yanga imecheza klabu bingwa, shirikisho na ligi kuu lakini Nkane hakutokea kuaminika na Nabi ila leo hii mnakuja kupiga kelele utafikiri huyo Nkane ni bora
 
Back
Top Bottom