Garama za kuanzisha radio

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
4,664
Reaction score
9,929
Poleni na majukumu wadau naimani kwenye wengi hapalibiki jambo

naomba kuuliza hivi kuanzisha radio ambayo itakuwa inadikika kilometa 100 kutoka mashariki magharibi, kusini na kaskazini inaitajiki shilingi ngapi
.asa

asanteni natanguliza shukrani
 
Poleni na majukumu wadau naimani kwenye wengi hapalibiki jambo

naomba kuuliza hivi kuanzisha radio ambayo itakuwa inadikika kilometa 100 kutoka mashariki magharibi, kusini na kaskazini inaitajiki shilingi ngapi
.asa

asanteni natanguliza shukrani

Mkuu bei ya coverage ya kilomita 100 inategemeana na wewe unataka vifaa vya daraja gani. Kuna vifaa vya low cost stations unaweza kukuta mixer unaipata kwa laki sita tu lakini kwa vifaa vya commercial radios au hata tu vya radio zenye mlengo wa kibiashara mixer unaweza kununua hata ya milion 17 unaona hiyo tofauti?


Sasa basi guarantee hapa ni budget yako tu uliyonayo, vinginevyo upande wa vifaa vya urushaji matangazo angalau set ya Transmitter, STL utahitaji kutenga angalau Tshs 50million na upande wa vifaa vingine tenga hata 15million. Jumla million kama 65m. Makadirio tu haya ya kawaida.

Una leseni?
Serikali kupitia TCRA imebadilisha utaratibu wa kuomba leseni na masfa ya radio ambapo zamani ilikuwa wewe mwenyewe ndiyo unaomba wakati wowote tu unapojisikia. Lakini kwasasa ni mpaka serikali itangaze kupitia TCRA kwamba kuna tender 5 za masafa ya radio, sehemu fulani, na sehemu fulani. Tatu za kibiashara mbili labla non commercial.
Ndiyo mnatuma maombi sasa kupambana na vidume wengine mbalimbali.

Kama unamalengo ya kuanzisha radio, weka focus hapa kwanza kaa mkao wa kula subiri tender kwanza.

Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…