Gari aina FunCargo unaweza kuilinganisha na Toyota IST au Raum?

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Kuna dogo kaniambia nikimnunulia Raum au Ist tunaweza kufanya biashara ya uber na akalaza hesabu fresh bila wasiwasi sasa kuna jamaa yangu mmoja ana Funcargo anataka aniuzie ila mm sio mzoefu saana wa magari hebu wajuzi nijuzeni tofauti ya hayo magari yani:

1. Funcargo

2. Raum

3. Toyota ist.

Shukrani.
 
Hesabu atalaza ngapi kwa siku ili tukushauri gari yenye consumption poa.
 
Raum zipo model ya zamani na new ni gari zuri.IST ni gari zuri pia ila funcargo ni old model. Cha muhimu jua kwanza hali ya engine na ulaji wa mafuta then mengine yatafuata maana mwisho wa siku unahitaj hesabu na uber kipato ni kidogo asikudanganye mtu yeyote so unahitaj kuwa na gar inayotumia mafuta kidogo na yenye running cost kidogo hapo angalau faida utapata ila vinginevyo utaishia kuwa chizi tu!!!
 
IST kubwa lao asee.
Zile gari ni chuma cha reli.
Katika gari naziamini mia ya mia ni IST na CARINA TI ni mkataba asee kwa gari ndogo
Carina TI zaidi kuliko hizo alizotaja na bei zinakaribiana, kwa biashara ya Taxie TI ni nzuri zaidi maana ina nafasi kubwa ndani na buti pia kwa mizigo ya abiria. Shida ya TI ni kupendwa na wezi kama polisi na maandamano ya CHADEMA.
 
Raum iko vizuri kuliko hizo gari zote. Hata mafuta haibwii maana ina 1500cc inafaa pia kwa ling safari sababu ni nzito na inashika njia
 
Hapana huwezi fananisha FunCargo na Ist. FunCargo= platz = vitz wamebadilisha body tu kila kitu kiko sawa. Engine, dashboard na zote ni cc 1000.

IST ipo vizuri zaidi kwenye kutulia barabarani na ukubwa na engine.
 
Napata wakati mgumu kwakuwa kila mmoja analisifia gari analoliendesha na si uhalisia wa gari zenyewe.
Hebu tu-neutralize kidogo.
 

Hali ya engine unaijuaje mkuu?
 
Google pana majibu sahihi, wengi wanatetea magari 'yao'
 
IST kubwa lao asee.
Zile gari ni chuma cha reli.
Katika gari naziamini mia ya mia ni IST na CARINA TI ni mkataba asee kwa gari ndogo
Mkuu naendelea kujiamini zaidi niendeshapo haka kagari kangu carina ti
 
Hapana huwezi fananisha FunCargo na Ist.
FunCargo= platz = vitz wamebadilisha body tu kila kitu kiko sawa. Engine, dashboard na zote ni cc 1000.
Ist ipo vizuri zaidi kwenye kutulia barabarani na ukubwa na engine.
hizo funcargo za cc 1000 utakuwa umetengeneza ww funcargo zimeanzia cc 1300
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…