Gari aina ya TOYOTA DCM kama wameshindwa kutoa new version itakayoendana na wakati, zitolewe katikati ya jiji la Dar

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Salaam wanajukwaa.

Moja kwa moja kwenye mada, wote tunaelewa hizi gari ni ngumu sana na zinapita mahali popote.

Kwa usalama wa raia (abiria) tunaomba mamlaka husika iziangalie hizi gari pamoja na magari mengine yaliyochoka sana.

Tunajua usafiri wa DSM ni mgumu sana lakini kila siku gari hizi zinakata break na kuhatarisha maisha ya watu

Mfano wa kwanza njia ya banana, kitunda, mpaka kivule na machimbo serikali kupitia Latra angalieni kwa jicho la pili hali ya magari yaendayo huko.

Mfano wa pili; Gongo la mboto kwenda majohe kwa ngozoma, halisi hadi viwege kwa mpemba kwa kweli magari yanayoenda huko ni kudra za mwenyezi mungu tu na uzoefu wa madereva.

Naomba kuwasilisha.

Habari bila picha ni umbea, kula chuma hicho.

images.jpeg
images (1).jpeg
 
Naunga Mkono hoja.
Njia ya Banana mpaka Frem 10 kuna Gari chakavu Mno na serikali inaona imekaa kimya.
 
Salaam wanajukwaa.

Moja kwa moja kwenye mada, wote tunaelewa hizi gari ni ngumu sana na zinapita mahali popote.

Kwa usalama wa raia (abiria) tunaomba mamlaka husika iziangalie hizi gari pamoja na magari mengine yaliyochoka sana.

Tunajua usafiri wa DSM ni mgumu sana lakini kila siku gari hizi zinakata break na kuhatarisha maisha ya watu

Mfano wa kwanza njia ya banana, kitunda, mpaka kivule na machimbo serikali kupitia Latra angalieni kwa jicho la pili hali ya magari yaendayo huko.

Mfano wa pili; Gongo la mboto kwenda majohe kwa ngozoma, halisi hadi viwege kwa mpemba kwa kweli magari yanayoenda huko ni kudra za mwenyezi mungu tu na uzoefu wa madereva.

Naomba kuwasilisha.

Habari bila picha ni umbea, kula chuma hicho.

View attachment 3148063View attachment 3148064
Nilitaka kukuunga mkono ila nilipoona picha ya MTUKUFU MAFUGULI TU KWENYE HIYO GARI ...BASI NIMESEMA HIZO GARI ZIENDELEEE KUCHAPA KAZI TU
 
Ndo jiji kubwa la biashara hilo. Magari ya usafiri utadhani mafungashio ya mashudu.
 
Ili serikali izipige marufuku sharti barabara zitengenezwe. Hakuna tajiri atakayepeleka gari yake nzuri kwenye barabara mbovu vinginevyo route itakosa usafiri na wakazi wa maeneo hayo kuathirika zaidi.

Kwa ubovu huo bado magari hayo ni msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom