Mkuu, inaitwa Honda Vezel aka Honda HR-V.
Ina generation mbili, ya kwanza ni ya zamani sana ata sijawahi kutana nayo ila ya pili kuanzia mwaka 2014 nimeiendesha.
Kuna engine tofauti tofauti ila mi niliyoendesha ni cc 1500 Hybrid.
Baadhi ya picha kutoka Google.
Kwa umbo, sio kubwa sana wala sio dogo sana. Imemzidi IST kidogo, inataka kufanana na Dualis kwa umbo. Mfano, fananisha hapa shape na Rav 4 mnazoita Miss Tanzania.
Rav 4 iyo rangi nyigine sijui rangi gani ila Vezel iyo nyeusi.
Bei yake kidogo sio haba, bila ushuru tu huwezi pata chini ya million 18.
Bado hazijawa nyingi kwahiyo spare usitegemee kwenda dukani na kuikuta ila Dunia sahivi kijiji swala la spare ilikua zamani sio leo.
Kama uko vema kiuchumi nashauri ichukue tu.
Sitachoka kusema:
Kwa bei za mafuta zinavoenda, Hybrid cars ndio tunakoenda.