Gari gari lenye ladha nzuri ya kuendesha?

Papa Mopao

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2009
Posts
4,153
Reaction score
2,647
Samahani lakini kwa vile nimeleta mada ya kitoto, lkn ningependa kufahamu gari ambalo dereva akiliendesha huwa anafeel utamu kuendesha gari, sasa ni gari gani wewe kwa uzoefu wako unahisi ni tamu haswa hata kama umeendesha magari 100 katika maisha yako?
 
Maserati

Lamborghini

Ferrari

He he he ukimbie mwenyewe.
 
Kila mtu anahisia tofauti utamu Wa kuendesha unatofautiana kuna watu wanapenda akiendesha akae tu astarehe asishughulike auto cruise control nk, na juna watu Kama mimi gari ilinienjoy lazima liwe manual shift big exhaust kwa performance tuned engine rest arm kwa safari Za mbali
 
Sijaona gari linalokuwa tamu ukiendesha ama wewe unamaana nyingine ?
 
Una maanisha gari kweli au hii ni tafsida? Kama kweli unamaanisha gari, kila mtu ananunua gari kulingana na uwezo wake, au anaendesha gari kulinga na aina ya marafiki alionao, maana wanaweza kumwazima. Siwezi kusema uzuri wa kwa hiyo kila mtu atakupa jibu kulinga na gari alilowahi kuendesha either la kwake au la rafiki yake. Hapo huoni kama utapata majibu mengi.
 
kitu chenye cc kidogo km carina ndo kitamu na ladha nzuri kuendesha
 
Ukitaka gari lenye ladha nunua tamu ni kutoka Germany! Mecedes Benz, Audi, BMW au VW ( Toureg)
 
Nina enjoy nikiendesha trekta hasa likiwa limefungwa tela kubwa na lina mzigo.
 
gari tamu upate gmama la ukweli, ila wengine wanapenda vipotable.
 
Gari ili liwe tamu kwanza lazima uwe na hamu nalo kwa maana ya kuhamanika. Ushanifahamu? Wataka lenye turbo au 4X4? Lenye ujazo mdogo au mkubwa? Liwe na sauti wa kuliendesha au kimya kimya? Liwe refu au short chasis? Wataka la kuingiza gia au free style aka automatic?
Pia waweza kuvutiwa na rangi ati? Labda nyeusi? au chanikiwiti? Au penginepo wataka la hudhurungi au samawati yakhe. Ni jinsi tu unavyhamanika nalo
 

Mercedes Benz AMG 55
 
Ukitaka gari lenye ladha nunua tamu ni kutoka Germany! Mecedes Benz, Audi, BMW au VW ( Toureg)

na ukitaka upate hii feeling ya hizi germany cars lkn kwa bei nafuu sana, endesha Honda
 
Bajaj mayai mwisho wa mchezo... fresh air all the way!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…