Gari hairudi reverse

Mkuu gari hii ilikua inatumiwa na madereva zaidi ya mmoja kipindi hicho Mimi nilikua bado sijajua gari Ila baada ya kujua gari ndo likaanza Hilo tatizo

Ila tatizo ni transmission fluid waliweka sio yenyewe daah na imeua clutch plate
 

Nilikuwa tight sana kazini leo. Je umeimiliki hii gari wewe tangia ije tokea kwa mabeberu?

Hapo kwenye gear lever hakuna maandishi yaliyofutika? Angalia picha niliyotuma nadhani hii yako ilikuwa na R, 1,2,3, na 4 mahali.

Pana kitu model code yaweza kuwa kama hizi hapa:

ACA31-AWXGK yaani Rav 4 G
ACA31-AWXSK yaani Rav 4 S
ACA31-AWXXK yaani Rav 4 X

Unaweza hakikisha kwenye kadi kama wameonyesha? Au kwenye gari (hodi) itakuwa Rav 4 G, S au X?

Je gari hii ni:

Engine: 2AZFE, 5 Seater, 2400cc?

Tuanzie hapo tena.
 
Mkuu gari hii ilikua inatumiwa na madereva zaidi ya mmoja kipindi hicho Mimi nilikua bado sijajua gari Ila baada ya kujua gari ndo likaanza Hilo tatizo

Ila tatizo ni transmission fluid waliweka sio yenyewe daah na imeua clutch plate

Ilikuwa vizuri kujiridhisha kabla ya conclusion.

Provide chassis number and year of manufacture.

Preliminary tu- rule out ATF issues ambazo ni simple and cheaper.
 

yes ni 2AZFE ya 2390Cc

hakuna kitu kimebadilika kwenye gea
 
hakuna information yoyote zaid ya mwaka ma chassis

Ok.

Ainisha haya:

1. Unayo kwa muda gani gari hii sasa?

2. Kuna button ya overdrive. Unajua kama iko pressed ndani au iko nje?

3. Kuna dip stick ya transmission fluid kwa maelezo yako yaonyesha hauna uhakika ilipo. Please confirm.

4. Confirm transmission fluid haijabadilishwa tangu gari ije.

5. Gari imetembea km ngapi?
 

1. gari ipo miaka 4 sasa
2. Hakuna Button ya OD
3. Hakuna Deep stick ya Gearbox
4. ATF nilibadilisha 8 months ago Niliweka T4
5. Mpaka sasa Km ni 70,XXX
 
Kwanini unadhani gari yako ina gear 7?

Mkuu pana vitu kidogo zaidi vya kufanyiwa verification Ila:

1. Bila shaka gari yako ni 4 gears (japo yaweza kuwa 5 gears pia). Hapa tuta discuss kidogo zaidi.
2. Haipo AT gearbox isiyokuwa na Overdrive button.
3. Haipo AT gearbox isiyokuwa na dip stick.

#2 na #3 ni lazima zifahamike zilipo. #3 itakuwezesha kupima level. Inaweza kuwa una too much or too low ATF. Hii inaweza dhuru hata gearbox yako.

Overdrive button ikiwa haiko pressed huwa in Overdrive off - mode. Hapo huwezi pata gear za juu in your case gear #4. Inaweza fanya inavyofanya sasa hivi. Yaani RPM itaongezeka bila kubadili gia kwenda hiyo ya topmost.

Matokeo yake unaweza ishia around 60km/h to around 70km/h.

Ushauri nenda garage yoyote waulize wakuelekeze zilipo:

1. Transmission fluid dip stick.
2. Overdrive button yako.

3. Wakusaidie kupima level ya transmission fluid.

Hawawezi kukudai pesa kwa hiyo minor information.

You may be in the right direction to resolve this problem.

Please let me know.
 
Kwanini unadhani gari yako ina gear 7?

Vipi uliweza kufuatilia? Kama nilivyokwandikia haipo yoyote AT gearbox isiyokuwa na dip stick. Kwani bado hata ilivyo badilishwa hiyo fluid kipimo gani kilitumika ku replenish?

Jingine Rav 4 hiyo yaonekana kutumika Dextron VI.

Hivyo ni vizuri kuhakikisha unayotumia ni compatible.

Hata hivyo nakazia kufanya kwanza niliyokushauri kwenye hilo bandiko la awali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…