Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #41
Gari gani limekuwa kama mganga wa kienyeji!? Kila siku.. lete kuku, lete mayai, lete mbuzi pacha, mara lete vifaranga vya kijani.. kwenda halendi limebakia kuunguruma tu!! Mwisho watu wanaanza kudandia madaladala hivi hivi!!
Belinda.. unajua wakati mwingine hadi uwe na gari kwa muda fulani ndio unajua uzuri wake na matatizo yake. Kuna watu wengine hawaoni ugumu kutumia kiasi chochote na kwa namna yoyote kulihudumia gari lao ili kuhakikisha linaendelea ndio maana nimewahi kupita kijiji fulani nikakutana na jamaa wanaendesha "kombi" ya 1960 na linadunda tu! Cha kushangaza waliokuja na magari yao haya ya kisasa mengine hata mwaka hayakumaliza!