Gari inazima nikiwasha AC

Kumbe na mijapan ina shida [emoji3][emoji3]
Taabu ya hizi model za zamani kidogo za toyota mfano kuanzia mwaka 2004 kurudi nyuma,
Si rahisi kuonyesha check engine...
Ukiona check engine, jua tatizo limeshazaa wajukuu..
Baadhi ya watu wanajifariji kuwa toyota haziwashi miti ya Xmass....kumbe virusi vinazitafuna in background mode..
 
Dah mkuu hili bonge la shule. Hizi compressor clutch nje kama ulivozitaja kipumbu ndio mafundi wengi sana wana tu advise huku mtaani.
Utasikia wanasema ziko repairable tofauti na hizo nyingine.
Kuna gari hapa nikiwasha ac nikatembelea umbali fulani afu niki off gar. Baadaye nikiwasha tena haita waka. Dizaini kama inanyonya betri yaani mpaka uiwache kwa masaa fulani ndio itakubali kuwaka.
Je kuna mahusiano kati ya ac na betri ya gari?
Tatizo huenda likawa nini mtaalam?
 
Reactions: amu
Sorry, gari yako ulitoa compressor ya umeme ukaweka hii ya kawaida ya external clutch (fixed displacement compressor)? Kama jibu ni ndio, basi huwa kuna relay inafungwa ku-amplify voltage to 12v ili kuipa coil ya umeme wa kutosha kutengeneza usumaku kuweza kubana clutch ya compressor.. sasa kinachotokea ni hizo relay watakua wameunga vibaya so ina lead to parasitic power draw pindi gari inapokua off...yaan umeme unaendelea kuingia kwa relay kwakua power feed wire inatoka moja kwa moja either kwenye battery or positive wire inayotoka kwa alternator...so watakiwa wiring ya ac yako ikafanywe upya na kazi itakua nzuri.
 
Naona gari za japana zina shida zaidi. Pita kwenye garage zetu 95% ni gari kutoka japan
Hivi Tanzania gari nyingi Barabarani ni za wapi kama siyo Japani, upite gerage ukute gari nje ya Japani zimejaa wakati barabarani ni chache. hiyo sawa uende geraje za kenya alafu utegemee kukuta toyota nyingi kuliko nissan.
 
Mafuta kidogo, weka kuanzia lita 30 ili AC izoee!

Achana na mafuta ya elfu 5.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…