Gari kudondosha maji kwenye bomba la moshi

Gari kudondosha maji kwenye bomba la moshi

babkaju3

Senior Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
118
Reaction score
94
Habari wa jamii naomba kufahamu kuhusu gari kudondosha maji kwenye bomba la moshi haswa asubuhi nikisha iwasha ila baada ya saa 1 inakata hii inatokana na nn

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchanganyiko wa mafuta na hewa(charge) unapoungua kwenye chambers za cylinder huwa kuna mvukishaji(evaporation),ambayo matokeo yake ni kutengenezwa kwa hayo majimaji unayoyaona,injini ikiwa na joto la kutosha majimaji haya hukauka Mara tu baada ya kutolewa,au hukauka wakati yanasafiri kwenda nje ya gari kupitia bomba la moshi.

Wakati wa asubuhi injini na bomba ya moshi linakua halijapata joto kiasi cha kufanya haya majimaji yakauke baada ya kutolewa nje ya cylinder hiyo kiasi chake yanafanikiwa kusafiri hadi nje ya bomba na ndio hayo unayaona asubuhi hapo,ila baada ya injini kupata joto lake stahiki,na bomba kupata joto yanaacha sababu yanakauka kabla hayajatoka nje.

Pambana na hali yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchanganyiko wa mafuta na hewa(charge) unapoungua kwenye chambers za cylinder huwa kuna mvukishaji(evaporation),ambayo matokeo yake ni kutengenezwa kwa hayo majimaji unayoyaona,injini ikiwa na joto la kutosha majimaji haya hukauka Mara tu baada ya kutolewa, au hukauka wakati yanasafiri kwenda nje ya gari kupitia bomba la moshi...
Umejibu kiufasaha sana ndugu hili ndilo jibu sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CH4 + 2O2 = CO2 +2H2O
Mafuta yanayounguzwa kwenye gari lako yana nature ya Methane gas CH4 kwa hiyo yakiunguzwa kwenye uwepo wa hewa na sparks or light huzalisha Carbon Dioxide na Water vapour kama equation hii hapo juu inavyoonesha.

Gari inapokuwa nzee, muunguzo wa mafuta unakuwa haukamiliki vizuri hivyo kutoweza kuzalisha maji kwa wingi na ndio maana magari mazee Ulaya hayatakiwi kwa kuwa kama gari haizalishi maji ina maana inakuwa inachafua mazingira.
 
Ninachoelewa gari likitoa maji kwenye exhaust pipe ni dalili njema kwa engine yako.

Tena mafundi watakuambia engine ni nzuri.

Kimantiki sijui ni kwanini.
 
Ninachoelewa gari likitoa maji kwenye exhaust pipe ni dalili njema kwa engine yako.

Tena mafundi watakuambia engine ni nzuri.

Kimantiki sijui ni kwanini.
Hata mimi niliambiwa hivyohivyo pindi nivyokua nanunua ila nilipuuzia nikafikiri maneno ya dalali wananiset, nilivyowasha akaniita akaniambia unaona haya (maji yalikua yanatoka kwneye exhaust)? Engine bado iko poa. Nikaitikia ila sikujua maana yake.
 
Hata mimi niliambiwa hivyohivyo pindi nivyokua nanunua ila nilipuuzia nikafikiri maneno ya dalali wananiset, nilivyowasha akaniita akaniambia unaona haya (maji yalikua yanatoka kwneye exhaust)? Engine bado iko poa. Nikaitikia ila sikujua maana yake.
Ni kweli ankol.

Nadhani ndivyo ilivyo. Kwenye exhaust mvuke huwa unatoka ila kwa sababu gari linatembea huwezi ukaona.

Mara nyingi maji hutoka kwenye exhaust asubuhi wakati kuna ubaridi.

Na yanakuwa ni maji kama maji. Kama yanatoka maji na oil, au rangi ya maziwa,
basi peleka gari kwa fundi. Lakini maji kama maji hayana tatizo. Mara nyingi yanakuwa machache.

Wakati wa jua Kali sio rahisi kuyaona hayo maji.
 
Mchanganyiko wa mafuta na hewa(charge) unapoungua kwenye chambers za cylinder huwa kuna mvukishaji(evaporation),ambayo matokeo yake ni kutengenezwa kwa hayo majimaji unayoyaona,injini ikiwa na joto la kutosha majimaji haya hukauka Mara tu baada ya kutolewa,au hukauka wakati yanasafiri kwenda nje ya gari kupitia bomba la moshi...
umejaribu kwa kiasi chako



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom