Gari kutema cheche za moto kwenye bomba la kutolea moshi

Gari kutema cheche za moto kwenye bomba la kutolea moshi

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Hii si mara ya kwanza naona hili, tukio ni zaidi ya mara tano kwa gari kutema cheche za moto kwenye lile bomba la kutolea moshi nje (exousite) yaani cheche kama zile za mashine ya welding wakati wa kuchomelea.

Nimejaribu kuuliza sijapata majibu ya kuridhisha hivi huwa ni tatizo au ni kawaida maana nimepatwa na mshtuko isijekuwa linawaka ndani kwa ndani.

Naomba kama kuna wajuzi mnifafanulie tatizo ni nini
 
Gari ya petr0l bila shaka
Hata liwe la Diesel nalo lawez kutoa cheche.. Hii hali inatokea hasa kama umesafiri umbali mrefu na ambapo masizi yanaungua sana kwenye lile bomba la kutoa moshi na ukifika sehemu ukapiga lesi basi huo uchafu unaoungua hutoka nje kama cheche za welding
 
Hii si mara ya kwanza naona hili, tukio ni zaidi ya mara tano kwa gari kutema cheche za moto kwenye lile bomba la kutolea moshi nje (exousite) yaani cheche kama zile za mashine ya welding wakati wa kuchomelea.

Nimejaribu kuuliza sijapata majibu ya kuridhisha hivi huwa ni tatizo au ni kawaida maana nimepatwa na mshtuko isijekuwa linawaka ndani kwa ndani.

Naomba kama kuna wajuzi mnifafanulie tatizo ni nini
ha ha ha ha ha unamaanisha gari jpm au? [emoji23] [emoji23] [emoji23] bado wacha tuendelee kuisoma nambaa!!!!
 
Inawezekana kuna tatizo kwenye cooling section...ile sehemu pana kwenye muffler maana pale ndipo exhaust gases hupotezea na bad noises hupunguzwa
 
Ni "carbon deposit "kwenye bomba la kutolea moshi, hii hutokea baada kaboni hizo kuwa zimenaswa, sasa gari inapotembea moshi huwa unazipasha moto mpaka zinakuwa zinawaka, ndo maana huwa zinadondoka zikiwa na chembe chembe za moto (cheche). Usiku ndo unaweza kuzishuhudia vizuri.
 
Hebu weka details za hiyo gari, siku hizi magari mengi sanaaa mengine yanawekewa mifumo ya hvyo na mengine yanatoa mpaka moto kabisa, mfano mzuri ni subaru
 
Hiyo imaitwa fireback usiogope. Kwa magari makubwa makubwa kama subaru yanatoa moto kabisa acha hizo cheche.
 
11ebd0e65423f5437c22b0fe790a7b2d.jpg

Kama hivi
 
Gari kutoka moto inategemea hio gari imefanywa nini, wengine wanafunga flame thrower kwa ajili ya show off, nyengine huwa ni kwa sababu gari ipo tuned for high perfomance usage, nyengine huwa na tatizo la kutochoma mafuta vizuri kusababisha mabaki ya mafuta kukaa katika pipe ya exhaust na kuwaka
 
Back
Top Bottom