Gari kuua dif

Gari kuua dif

godson group

Member
Joined
Mar 10, 2017
Posts
21
Reaction score
6
Wakuu nina gari aina ya suzuki carry caburator kila baada ya miezi 8 hadi kumi lazima iue dif ya nyuma cjui tatizo ni nn
 
Wakuu nina gari aina ya suzuki carry caburator kila baada ya miezi 8 hadi kumi lazima iue dif ya nyuma cjui tatizo ni nn

Diff kufa ni kwa aina mbili: ama bearings zinakufa, au meno ya gears yanavunjika. Kwa bearings kufa ina maana kuwa huenda huweki oil inayotakiwa, ukiweka Engine oil za karibia 10W-30 badala ya gear oil za kiwango cha 80W-90, basi gearbox itapata joto na kuua bearing zake baada ya muda fulani. Meno ya gear yanaweza pia kuvunjia kwa sababu hiyo hiyo ya oil, lakini pia kama hakuna clearance ya kutosha baina ya meno ya gear; fundi lazima atumie feeler gauge kupima clearance ile wakati meno yakiwa baridi. Kama yamebanana sana, basi yatavunjika yakipata joto, na vile vile kama clearance ni kubwa sana utakuwa unasikia backlash wakati wa kuanza safari au wakati wa reverse, hiyo pia inaweza kusababisha meno ya gear zile kuvunjika kutokana na impact ya mara kwa mara (fatigue). Zaid ya sababu hizo mbili ni kuwa labda Oil seals huwa hazifungwi vizuri na hivyo kuvujisha oil yote, jambo ambalo husababisha baadaye bearings nazo zife.
 
Back
Top Bottom