Ni kitu gani hasa kinachotetemeka, gari zima au usukani? Nilienda safari siku chache zilizopita, kila nikifika mwendokasi wa 100-110kph, usukani unatetemeka sana, nikifika 120kph, unatulia. Baada ya kufika, nili Google, nikaona wanashauri kufanya wheel balancing, siku 5 kabla ya safari nilifunga tairi zote mpya. Nilipoenda kwenye wheel balancing, matairi yote yalikuwa out of balance. Baada ya kurekebishwa, nilifika hadi 140kph bila kuhisi mtetemo wowote ule kwenye usukani. Zingatia hilo pia. Endapo ungekuwa ukipunguza mwendo ndio unasikia mtetemo, hiyo ingekuwa kuna shida kwenye calipers.