Gari kuwa na nguvu zaidi ya ile niliyoizoea

Master C mimd

Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
46
Reaction score
55
Habarini wana jamvi

Katika mihangaiko yangu leo asbhi niko na drive mara kwenye dashboard taa ya AT OIL TEMP ikawaka (ilitoke baada ya kuweka sport mode kipindi na overtake). Nikawasiliana na fundi nikaipeleka gari sehemu husika, wakabadili oil ya gearbox na pia kuna kifaa walikifanyia usafi pia.

Sasa baada ya wao kumalizi nikaichukua ndinga yangu kuendelea na mizunguko yangu kitu nilichoona cha tofauti ni kuwa nikiweka D tu gari inaanza kutembea kwa speed ambapo ni tofauti na mwanzo, nimejaribu kuwasilian na fundi amesema ni kawaida hiyo hali maan ndivyo gari inavyotakiwa kuwa

Nimekuja kuomba ujuzi na mawazo zaidi, je fundi yuko sahihi? Au kuna sehemu tena itakuwa iliguswa? (Car type ,Subaru impeza 2009)
 
Mkuu unampa funguo atengeneze au unasimamia service za gari yako. Kuna wengine huwa mnatoa tu ufunguo na hujui wala uhoji nini na kipi kumebadilishwa.

Wenzio tunanunua wenyewe oil husika na hizo filter na inampa fundi abadilishe tu.
Any way una fundi mtiifu.
 
Gari lako kaa gear box haina matatizo, kama umepak gari sehemu tambarare, ukiweka D ukaachia brake gari linatakiwa liondoke taratiibu wakati rpm inasoma kati ya 0.5 mpaka 1k na si zaido ya hapo..
na speed ya gari inatakiwa iwe ndogo mathalani si zaidi ya 10 kph.

Sasa gari lako kama ukiweka D linakimbia zaidi ya speed 10 huko kuelekea 30+..
Kwa kweli hapo sielewi.

Wajuzi zaidi wataelezea
 
Same problem.
Rpm inasoma 20kph.
Ikiwa silence
Rav4V kilitime
Hio uloandika sio RPM ni speedometer. Kachekishe Sensor za speed kama zipo sawa na hio cluster.
 
Reactions: 1gb

Asante kwa mawazo yako
 

Nimekuelewa mkuu
 
Nini kinachangia kupanda silencer ikiwa iddle.

Kuna gari ya jamaa alishusha silencer mpaka 700.

Ila asubuhi akiwasha gari, silencer inapanda yenyewe mpaka 1200 halafu inarudi yenyewe taratibu mpaka 900 na sio 700 iliyowekwa awali.
 
Subaru zote ziko hivyo ukisafisha throttle Tu engine inakuwa na nguvu mno nakumbuka subaru forester ya jamaa Yangu alisumbuka nayo Sana Kwa mafundi makanjanja mpaka alivyoenda Kinondoni Biafra garage ndipo gari ilitulia,
Tena gari yake ilikuwa inawaka taa ya check engine muda wote....
 

Kweli mkuu.....nimeona hicho kitu
 
Nini kinachangia kupanda silencer ikiwa iddle.

Kuna gari ya jamaa alishusha silencer mpaka 700.

Ila asubuhi akiwasha gari, silencer inapanda yenyewe mpaka 1200 halafu inarudi yenyewe taratibu mpaka 900 na sio 700 iliyowekwa awali.
Huwa ni kawaida kwa asubuhi ukiwasha gari silencer inakuwa juu kuna magari inaweza kufika mpka RPM 3000 kisha inashuku taraatibu mpaka kufikia Kati ya 500 mpaka 1000 hivi.....

Ikiwa inachezea hapo kwenye 500 mpaka 1000 siyo mbaya kutegemea na aina ya gari pia....
 
Hii ni experience nzuri sana. ...
Haya ndiyo mambo yanayotakiwa watu kushare pamoja...

Ukipata tatizo fulani unaelezea namna lilivyotibiwa inasaidia wengine wanaomiliki gari la aina hiyo..

Nachukia sana wale watu wanasema tu...gari fulani majanga...anaishia hapo haelwzi kwa kina matatizo ya gari husika na namna ya kuyatatua
 

Ni kweli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…