Jamani,
Nimesoma na kuona picha ya ajali ya bajaji na gari taka iliyotokea siku ya wapendao na kuua mama na mtoto wake wa miaka mitatu( viewer discretion is advised as the photos are not in a good state)Global Publishers - Picha
Jamani kwa nini manispaa zetu zinaruhusu na kupitisha kandarasi hizi kwa watu wenye magari ambayo si magari bali taka kubeba takataka jijini? Jamani hizi si ndio ufisadi wenyewe huu. Mkandarasi hana hata uwezo wa kuagiza gari la mtumba, anafufua lori la mwaka sabini na kuanza kulitembeza barabarani. Dar es salaam inaongoza kwa haya matakataka gari. Hayana break na hata sura yake ukiiona zaidi ya kuwekewa 'mkorogo' halifai hata kutembezwa kwenye barabara zetu.
Suluhisho: Idara ya usalama barabani inabidi ibadilishwe na kuleta wanausalama wanaojali utawala wa sheria.
Pili, kuna hili suala la manispaa zetu kutangaza zabuni na kuchagua wakandarasi uchwara, nafikiri inabidi kuwepo na usimamizi wa kudondokea (spill over supervision) kutoka takukuru, police na wale watu wa Procurement Authority hili kukwepa dhaama za hawa mabazazi wanaopitisha tenda kwa njia za ajabu ajabu.
Hitimisho: Hili suala limetokea nje ya ofisi za Halmashauri ya manispaa Kinondoni na mpaka sasa hakuna tamko lolote linalomhusu mkandarasi wao.
Mwisho, serikali kuruhusu bajaji na pikipiki bila kuratibu hao watu wanaokaa nyuma ya vyombo hivyo (madereva) naona ni kama utambi wa bomu umeanza kuungua.