Gari la msafara wa IGP Sirro laua Morogoro


Nimekutana na hiyo ajali maeneo ya makunganya kwa matraffick pale ni seme tu traffic pia hawakuwa makini kwani imetokea mbele yao hawakutoa taadhari abiria walioshuka kwenye gari.

Mtoto alirushwa juu dah RIP binti, inaonekana mama alikuwa naye ni mlezi na ndiyo alikuwa anamsomesha alimuwa analia sijui atamwambia nini mwenye mtoto.
 
Ukiachana na ajali Ni upuuzi, kero, na kutupotezea muda kutuweka kwenye folen kisa IGP....

WAPANDE HELIKOPITA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sad! Kwani lazima IGP akimbie kwa kasi bila kuchukuwa tahadhari? Driver aliyegonga hakuona basi na watu? Kwanini hakuchukuwa tahadhari kwa kupuunguza mwendo???????
Sent using Jamii Forums mobile app
 
*pole wafiwa

*meona basi la modern kwenda mombasa yamegongana na vifo vimetokea (mabasi ya kampuni moja yanagongana ...waeza waza na kukosa majibu)

mwaka unayoyoma ...19 days
 
Mtoto haachwi nyuma jamanii dah mnanikumbusha machungu ya mwangu
 
Mkuu Sirro sheria ni msumeno , nenda kituo cha polisi cha karibu ukaandike maelezo
 
Igp ashtakiwe kwa kusababisha ajali. Kwani hakuwaelekeza madereva wa msafara wake waendeshe kwa kuzingatia alama za barabarani? Awajibike!
Kwani IGP ndo alikuwa anaendesha hilo gari? Hadi ashtakiwe? Halafu toka lini IGP akawa muongoza magari ya msafara wake?
 
Ingekua ni dereva mwingine wa kawaida tu taarifa hiyo ya ajali ingeendelea kwa kusema "Dereva wa gari lililosababisha ajali anashikiliwa na polisi". Lakini hapo nadhani protokali itavunjwa
 
Kwani IGP ndo alikuwa anaendesha hilo gari? Hadi ashtakiwe? Halafu toka lini IGP akawa muongoza magari ya msafara wake?
Yeye ndiye msababishaji mkuu kwani bila yeye kupita hapo na msafara wake binti yule angekuwa salama! Na kwani atembee na convoy kana kwamba yupo Somalia? Gari mbili- zinamtosha kwenye msafara wake na siyo gari 10!
Wanasheria mnakwama wapi kupata kick kwa kumfungulia kesi huyu igp?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…