Mkuu nakushauri ondoa kabisa kwenye list yako gari aina ya NADIA, siyo gari kabisa mkuu. Gari yenye show nzuri ni Raum new madel ingawa siyo imara kama Raum old model. Ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana, cc 1490.
Gari ya kazi ni Toyota Probox japokuwa haina show nzuri sana kama raum but zipo baadhi zimenogeshwa. Probox zimetofautiana engine capacity, kuna zenye cc 1250 na cc 1490, ila no gari za kazi. Raum old model zinanguvu sana na huwa hazinasi hovyo mchangani. Raum Mafuta ya 10,000 unatoka kinyerezi mpaka mbagala na kurudi. Spare parts ni za kumwaga na bei Cher.
Uamuzi ni wako mkuu, tulia ufanye uamuzi sahihi ili usije jutia pesa yako.