Gari ya kubebea mizigo (van)

Gari ya kubebea mizigo (van)

Kileghe

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2014
Posts
367
Reaction score
315
Nawasalimu.

Nina biashara yangu ya duka hapa dar es salaam na Handeni Tanga, huwa bidhaa zangu nanunulia maduka mbali mbali kitumbini na kariakoo.

Nafikiria kununua gari itakayosaidia wakati wa kukusanya na kunisaidia kuibeba hadi sehemu husika( duka la Dar na Handeni) na pia itumike kama gari ya familia kwa safari ndogo ndogo.

Nimeona hizi gari mazda bongo van na nissan venette baathi ya makampuni ya hapa dar wanatumia kusambazia mizigo. Bei ya kuagizia kutoka japani nimeona ni kati ya milioni 9 hadi milioni 10 ambapo iko kwenye bajeti yangu.

Naomba mwenye uzoefu wa hizi gari tukizilinganisha na toyota noah, ubora, ulaji wa mafuta,kuhimili mzigo na safari, ukubwa wa bodi la kubebea mzigo,upatikanaji wa vipuli.
Mazda_Bongo_-_jpg.jpg

Gari hizi zinakuja za petrol 1780cc na za diseli 1990cc Pia ziko za 2wd na 4wd,zinapatikana za gia automatic na manual.

Napokea ushauri pia wa gari aina nyingine litakalokithi majukumu yangu kwa salio langu lisilozidi millioni 12 kwa kuongezea 2 milioni niliyoitenga kama dharula.

Aksante
 
Noah ni bora zaidi.
Aksante, kati ya hizi noah je kuna ambayo ni bora zaidi ya mwenzake kati ya hizi za mwaka 2006 na hizi za mwaka 2000 wanaziita liteace noah na nashangaa kwa bei ya kununulia japani hizi za mwaka 2000 n ghali kidogo ukilinganisha na hizi toleo la kati 2006
 
Back
Top Bottom