Gari yangu inatoa moshi mweupe mwingi kama wingu naomba msaada

Gari yangu inatoa moshi mweupe mwingi kama wingu naomba msaada

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
2,399
Reaction score
1,014
Tafadhali wataalamu na wazoefu wa jukwaaa letu pendwa

1.Gari yangu ilianza kutoa moshi mwingi kama wingu kubwa na ilikuwa inaonyesha engine check baada ya hapo nikabadilisha oil s40 na baada ya kuchange oil ikawa haitoi tens moshi kabisa na ile taa ya check engine ikazima Ila baada ya halo nikawa nimesafiri mpaka sasa Niko safarini mwezi sasa hapa sijui tatizo ndo limeisha kabisa la kutoa moshi au laa coz nilienda kama km 10 tu baada ya change oil na nikawa sijaona moshi wala check engine na kulipack until today SASA USHAURI WOWOTE NAUPOKEA gari yangu in spacio new model 4WD .GARI SIJASAFIRI NAYO NIMEIPACK NYUMBANI ALMOST MIEZI MIWILI SASA ILA BAADA YA KUBADILI OIL MOSHI HAUKUTOKA NA TAA YA CHECK ENGINE ILIZIMA ILA BAADA YA KUTEMBEA KLMETA 40 IKAWAKA NA MOSHI UKARUDI MWEUPE

2. Naomba kufahamu nikirudi mambo ya kufanya baada ya kurudi safarini baada ya kuiacha gari kwa zaidi ya miezi miwili na kwa kuwa nilipoiacha pana vumbi na mvua mvua hizi najua gari itakuwa imechafuka sana na nitumie sabuni gari nzuri ya kuoshea gari yangu irudi usafi na mngao nmzuri kutokana na mavumbi ya muda. Je, nioshee nini taa za gari zingaeee.

3.Je ni sahihi kumwaga oil ya gia box yote au in vyema kuongezea na ipi in sahihi kuweka sijawahi badili tangu miaka mitatu niliyonunua na je inatakiwa kubadilishwa baada ya km ngapi ?

Nawasilisha .
 
Duh!kwanza nikupe pole sana mkuu pamoja na yote uliyoyaelezea hapa hivi unafahamu kuwa oil ya gari au pikipiki huwekwa kulingana na kilometers kama unatambua ilo kwann hukufanya hivyo way back?

Haya upo safarini fahamu ufikapo safari yako cheza na kilometers ulizotembea ubadilishe tena iyo oil alafu unatumia oil gani na bei gani tuanzie hapo kwaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nijibu namba 3.
Ndio Badirisha. Weka ATF Type IV ambayo ndio recommend na Toyota. Utaipata wapi? Nenda Toyota office (kama upo DSM nenda Kariakoo mtaa wa Msimbazi) utauziwa Tsh 95,000Tsh (kama imebadirika ni kidogo) Lita zako 4 Safi.

Baada ya hapo utaona mabadiriko sana.

Namba 2
Peleka car wash tu mzee. Watakusaidia. Kuna car wash wanafua Hadi seat. Wanazitoa wanazipiga Maji.

Namba 1
Sababu zipo nyingi ila nahisi Oil itakua inavuja somewhere. Je, driving experience imebadirika kwa vyovyote? Yaani nguvu.
 
Mkuu usije ukawa ule moshi unakuwepo wakati exhaust ipo wet sababu ya hizi mvua zetu za hapa na pale
 
Niulize swali hili...
Je coolant/ maji ya radiator yanapungua mara kwa mara..?

Kama jibu ni ndiyo ni wazi kwamba gari lako linaunguza coolant/ maji kwenye combustion chamber...

Gari kutoa moshi mweupe usioisha ni ishara kuwa linaunguza coolant..

Moshi wa blue ni ishara kuwa linaunguza oil..
Angalia hayo mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh!kwanza nikupe pole sana mkuu pamoja na yote uliyoyaelezea hapa hivi unafahamu kuwa oil ya gari au pikipiki huwekwa kulingana na kilometers kama unatambua ilo kwann hukufanya hivyo way back?

Haya upo safarini fahamu ufikapo safari yako cheza na kilometers ulizotembea ubadilishe tena iyo oil alafu unatumia oil gani na bei gani tuanzie hapo kwaza

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Ila nimeelezea vyote hapo juu natumia s40 na kilichotokea nilimwazima mshikaji gari kwa mda wa wiki na alivyoirudisha akiwa hivyo na akawa ameichukuabkwenda nayo kwa funding ile nimemfuata nakuta kashaweka oil s40

Na pia kwa huku safarini sipo na gari hiyo.HIYO SPACIO NIMEIPACK TOKEA HAYO MATATIZO

Ila kwa sasa haitoi tena moshi sasa sijui tatizo lilikuwa ni oil tu au ni nini
 
Naomba nijibu namba 3.
Ndio Badirisha. Weka ATF Type IV ambayo ndio recommend na Toyota. Utaipata wapi? Nenda Toyota office (kama upo DSM nenda Kariakoo mtaa wa Msimbazi) utauziwa Tsh 95,000Tsh (kama imebadirika ni kidogo) Lita zako 4 Safi.

Baada ya hapo utaona mabadiriko sana.

Namba 2
Peleka car wash tu mzee. Watakusaidia. Kuna car wash wanafua Hadi seat. Wanazitoa wanazipiga Maji.

Namba 1
Sababu zipo nyingi ila nahisi Oil itakua inavuja somewhere. Je, driving experience imebadirika kwa vyovyote? Yaani nguvu.
Asante boss wangu kwa majibu yako makini sana.

Hakuna mabadiliko yoyote kwenye nguvu ya gari na pia toka imwagwe hiyo oil na kuweka hiyo s40sijaona moshi tena Ila sikulitumia gari baada ya hapo niliipack mpaka sasa toka mwezi wa pili sasa ndo nilikuwa nauliza tatizo litakuwa limeisha au laaa
 
Usisahau kucheck na Traffic pengine linadaiwa kwa makosa ya barabarani
 
Niulize swali hili...
Je coolant/ maji ya radiator yanapungua mara kwa mara..?

Kama jibu ni ndiyo ni wazi kwamba gari lako linaunguza coolant/ maji kwenye combustion chamber...

Gari kutoa moshi mweupe usioisha ni ishara kuwa linaunguza coolant..

Moshi wa blue ni ishara kuwa linaunguza oil..
Angalia hayo mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana nilikuwa natumia maji na ni kweli maji hupungua sana.SAMAHANI KIONGOZI NIFANYEJE NICHUKUE HATUA GANI ?
NA KUPITIA JUKWAA HILI NIMEPANGA KUTOTUMIA TENA MAJI YA BOMBA
 
Siyo asubuhi tuu ni siku nzima hutoa moshi kama wingu
Oil sahihi ya magari madogo ni 5w30 au 5w20, kama limeenda km nyingi ndo unashauriwa utumie 5w40.
Inaweza isikusaidie kwenye case hii ila inaweza kukusaidia kwenye issue zingine.
Ni vizuri ukawa na diagnosis tool ya gari lako, taa ya check engine huwa inalog kwenye ecu, kama unatool unaweza kujua kilichotatiza ni nini hasa.

Online Shop OBD2 ELM327 Automotive Scanner Bluetooth ELM327 V1.5/2.1 Car Diagnostic Code Reader Scanner Automotivo for Android | Aliexpress Mobile_en title

Mfano wa tool, zinatofautiana kwa ubora na kama utaopt hizo elm tafuta v1.5
 
Mkuu pole Sana kwa mawazo juu ya Gari lako..maana inaonekana huko ulipo roho IPO juu juu...huo Moshi huenda Ni kwa sababu ya hizo piston rings
 
Mkuu pole Sana kwa mawazo juu ya Gari lako..maana inaonekana huko ulipo roho IPO juu juu...huo Moshi huenda Ni kwa sababu ya hizo piston rings
Da ni kwelii akili yangu haipo sawa.Unaposema ring pistons imekufa sasa mbona haitoi moshi na check engine imezima baada ya kubadili oil.Au huwa ukibadili oil kama ring zimekufa inaacha kutoa moshi kwa mda then inaendeleaa ?tafadhali msaada na majibu yako ni MUHIMU SANA
 
Kama maji yanapungua mara kwa mara na kuna sababu kuu mbili..
1..Huenda kuna sehemu radiator inavuja, kama sivyo..

2...Maji yatakuwa yanavuja ndani ya engine na kuingia kwenye combustion chamber ndiyo maana unapata moshi mweupe kama wingu....

Sabau za maji/coolant kuingia kwenye combustion chamber
1...Head gasket inaweza ikawa inashida..
2... Cylinder head huenda imecrake/imepinda.
3...Block engine huenda imecrake...

Japi sababu ya 3 haina nguvu kama 1 na 2.

Tafuta mafundi wabobezi watajua cha kufanya.

Ukishapata ufumbuzi, achana na maji ya bomba nunua coolant kutoka kwenye maduka yanayoaminika au vituo vya mafuta.

Maji yanatabia ya kuozesha njia za ndani ya engine na baadae kuleta madhara...

NB kutumia SAE 40, hakufanyi gari kutoa moshi mweupe...moshi utatoka wa kawaida tu japo utakuwa unaichosha injini yako..

.
Asante sana nilikuwa natumia maji na ni kweli maji hupungua sana.SAMAHANI KIONGOZI NIFANYEJE NICHUKUE HATUA GANI ?
NA KUPITIA JUKWAA HILI NIMEPANGA KUTOTUMIA TENA MAJI YA BOMBA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh!kwanza nikupe pole sana mkuu pamoja na yote uliyoyaelezea hapa hivi unafahamu kuwa oil ya gari au pikipiki huwekwa kulingana na kilometers kama unatambua ilo kwann hukufanya hivyo way back?

Haya upo safarini fahamu ufikapo safari yako cheza na kilometers ulizotembea ubadilishe tena iyo oil alafu unatumia oil gani na bei gani tuanzie hapo kwaza

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa gari limepatwa.
Jamaa hajui maana service!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom