Gari yangu Toyota Rav4 inakula sana mafuta

kindoki

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2018
Posts
213
Reaction score
218
Natumia gari langu dogo Toyota rav4 lakin limeanza kula mafuta vibaya, naitaji ushauri wa kiufundi kwani nalipenda sana gari langu, nicheze na mfumo gani ili iwe inakula vizuri, gari lenyewe lina CC1998, mwanzoni lilikuwa na racial ya 1LTR for 8 KM.

Nahitaji msaada kwa mtu mwenye experience na hizi gari.
 
Nina fundi wangu ningekupa anachomeka laptop tu mambo shwari
 
Ugonjwa huu umekuwa ukiniumiza sana kiuchumi, gari ina cc1998, yaani ulaji wake cio wa kawaida, nifanyaje kwa wenye uzoefu na rav4
 
Nikiweka Lita 20 zinaisha kwa kutembelea km 30 tu
Kama umesema ni Lita 20(na siyo ya Tsh 20,000) kwa uchache hata kama gari ile vipi lazima kilometa 150 utoboe. Kwa mfano Brevis inakula mafuta kuliko Mark X,Verossa,Mark Grande,lakini kilometa 140 kwa lita hizo 20 unafika.

Hata hivyo ubaya wa RAV4 za mwaka 1995-97 hazikua na umeme mwingi,hivyo speed na power hutegemea utumiaji mafuta mengi. Mwaka 1998-2000, RAV4 walibadilisha na kuanza kuweka umeme. Kumbuka kuna old model hadi mwaka 2000(lakini hasa hadi mwaka 1999)! Mwaka 2000 walitoa chache na kutoa model mpya ya Kill Time(katika mifumo miwili Engine 1ZZ VVT-i, cc 1800 pia Engine 1AZ D4 cc 1990:2000 cc.

Tukirudi kwenye mada,RAV4 hizo huenda kilometa 7-8/L kama hakuna foleni. Kumbumba Lita 20 ni karibu 50,000(46,000)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…