Mpangamji
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 540
- 140
Leo nimeshitushwa na simu ya mtu niliyemtuma kwenda kununua gas kg 15 nikiwa nimempatia Tshs 55,000 lakini aliniambia kuwa gas ni Tshs 70,000 nilimwambia aache porojo, ndipo aliposisitiza kuwa bei imepanda, niliamua kuulizia sehemu nyingine ili nijue, nikaambia bei ni 70,000 kwa mtungi wa kg 15. tunakwenda wapi jamani, afadhali tuingie barabarani hawa watu tuwatoe madarakani, kwa mshahara wa 290,000 hii nini, chumba na sebure 150,000 kwa mwezi, gas 70,000 maji Tshs 300/dumu X dumu 5 X siku 30 = 45,000 daladala Tshs 700/siku x siku 20 = 14,000 mkate Tshs 500 x siku 30 =15,000 (294,000)
Mchele, unga, sukari, mafuta, umeme, mafuta ya kujipaka mwilini, kunyoa nywele, salon kwa wadada. tunakwenda wapi?????
Mchele, unga, sukari, mafuta, umeme, mafuta ya kujipaka mwilini, kunyoa nywele, salon kwa wadada. tunakwenda wapi?????