Gavana akerwa na utoro na kutowajibika kwa waalimu

Gavana akerwa na utoro na kutowajibika kwa waalimu

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
*~ Afanya ziara ya kushtukiza na kubaini Madudu*

Na Mwandishi wetu,

Afisa Tarafa Mihambwe, Gavana Emmanuel Shilatu amekemea vikali suala la utoro na uzembe wa kufundisha unaofanywa na Waalimu.

Gavana Shilatu aliyasema hayo wakati alipotembelea Shule ya Msingi ya Kitama ili kujionea hali ya ufundishaji ambapo katika Madarasa matano aliyotembelea ya shuleni hapo ni darasa moja lilikuwa lina Mwalimu anafundisha. Na kwa uchunguzi alioufanya Gavana Shilatu kupitia kuwauliza Wanafunzi maswali amegunduka ni masomo mawili mpaka matatu kati ya sita anayopaswa kufundishwa Mwanafunzi ndiyo Waalimu huingia Madarasani.

"Nimeshtushwa na kiwango hiki cha utoro na cha uzembe wa kufundisha kinachofanywa na Waalimu. Mwalimu Mkuu upo, Afisa Elimu kata upo na haya yanatendekea mkiyashuhudia pasipo kuweka nguvu na ukali wa kuyakemea. Hali hii iwe mwanzo na mwisho, nahaidi nitarudi tena kukagua, nisikute tena uzembe huu" alisema Gavana Shilatu.

Katika hali ya kuhakikisha Wanafunzi wanamudu kujibu vyema mitihani alishauri waanzishe mtindo wa kufanya mitihani ya ujirani mwema yaani shule na shule washindane.

"Nawapongeza kwa kununua photocopy mashine ya kisasa na komputa, tumieni vifaa hivyo vyema kwa kuanza mashindano ya kufanya mitihani ya ujirani mwema." alisema Gavana Shilatu.

Katika ziara hiyo ya kutembelea shuleni hapo, Gavana Shilatu aliambatana na Diwani wa Kata, Mtendaji wa Kata, Afisa Elimu Kata, Mtendaji wa Kijiji cha Kitama Shuleni na kupokelewa na Mwenyeji wao Mwalimu Mkuu wa shuleni hapo.
IMG_20181002_115400.jpg
IMG_20181002_120029.jpg
IMG_20181002_120905.jpg
IMG_20181002_120859.jpg
IMG_20181002_125001.jpg
IMG_20181002_121946.jpg
 
Hawajapandishwa madaraja,Cwt kimekuwa chama cha siasa,increment hakuna ,siasa imevamia taaluma,hatari
 
Samahani wakuu naomba kujuzwa shilatu inapatikana halamashauri gani?
 
Back
Top Bottom