Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Gavana wa Machakos Dr. Alfred Mutua, sasa anadai kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, amepunjwa kwenye muungano wa NASA na mgombea urais wa muungano huo Raila Odinga. Dkt. Mutua anadai kwamba ikiwa Raila atashinda uchaguzi wa urais, Kalonzo hatapata tiketi ya moja kwa moja ya kugombea urais wa muungano huo mwaka wa 2022 bali atapitia kwenye uteuzi. Dkt. Mutua alisema Kalonzo atakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea uchaguzi wa magharibi mwa nchi, ambako kuna idadi kubwa ya wapiga kura. Aliwaambia watu wa Ukambani kumpigia kura rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wakati wa marudio ya uchaguzi wa urais tarehe 17 mwezi Oktoba kwani jamii ya Ukambani itanufaika zaidi na maendeleo chini ya utawala wa Uhuru na Ruto.