BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Maria Maria alikwama kulipa deni la matibabu aliyopata baada kugongwa na gari wakati akitembea Barabarani ambapo alilazimika kubakia Hospitali ya Nakuru Level Five tangu Agosti 2022.
Gavana wa eneo hilo Susan Kihika amechukua dhamana ya deni lote baada ya ndugu wa Maria kutoonekana tangu alipofikishwa Hospitalini hapo na hivyo kukosa msaada. Ripoti ya matibabu kutoka hospitalini zilionesha kuwa alivunjika mguu wa kulia na kupata majeraha mengine.
Licha ya kudhaminiwa deni hilo, Hospitali haijamruhusu kuondoka baada kutojulikana atakapokwenda huku Maria mwenye miaka 47 akisisitiza kuwa familia yake iko Chato. Gavana huyo pia alitoa msaada wa Tsh. Milioni 97 na kulipa madeni ya wagonjwa 64.