Gavana ndulu inabidi ajiuzuru kwa kulitia taifa letu hasara ya mabilioni ya shillingi. alipokuwa akitoa sababu za kubadilisha pesa alisema pesa zilizopo inabidi zibadilishwe kwa kuwa hazina ubora na pili zinagushika kirahisi kwahiyo serikali imepata mbia atayetengeneza noti zingine zitakazokuwa na ubora wa hali ya juu na pia itakuwa vigumu kughushika. kulingana na taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi noti hizi mpya za kaniki ni rahisi kughushika kuliko za zamani na hazina ubora wowote kwani ukiziangalia zingine mirangi inachujika haraka na kuwa kama imepigwa pasi. kwa kuwa sababu alizozitoa za kubadilisha pesa zimekuwa ni kiini macho gavana inabidi aachie ngazi kwani ushauri wake umeliingiza taifa hasara kubwa za kubadili noti na pia kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara ambao tumekuwa tukipokea noti feki kwa wingi kila kunapokucha kuliko hapo zamani. umezipika mbiu wewe mwenyewe inabidi uzitafune na siyo kuwaachia wengine watafune kwa excuse zako za ajabu ajabu kwani tunachoangalia hapa siyo issue ya noti kughushiwa tu bali ni wingi wa noti kughushiwa kwani umeifanya kazi yao kuwa rahisi zaidi kuliko hapo mwanzo.