Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Gavana wa kaunti ya Kisumu Professor Anyang' Nyong'o ametangaza kufanya wamuzi wa kusitisha maandamano dhidi ya serikali, na badala yake ametoa rai kwa wananchi wa kaunti hiyo kuungana na wenzao walioko Jiji Kuu la Nairobi.
Kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Gavana Nyong'o amekiri kuwa uongozi wake pamoja na wakazi wa kaunti ya Kisumu watazidi kusimama kidete na Raila Odinga katika kushinikiza kushuka kwa gharama ya maisha pamoja na kufunguliwa kwa sava za Tume ya Uchaguzi IEBC kwa lengo la kung'amua ni yupi hasa alishinda kiti cha urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti mwaka jana.
Aidha Nyong'o, ambaye alichaguliwa kwa tiketi ya Chama cha Odinga ODM, amewashauri wakazi wa kaunti hiyo kushirikiana na vyombo vya usalama ili kuhakikisha amani na usalama inadumu ndani ya Jiji hilo.