Gavana wa Mombasa Ali Joho azuiliwa uzinduzi wa SGR, kufuatia uhasama kati yake na Rais

Gavana wa Mombasa Ali Joho azuiliwa uzinduzi wa SGR, kufuatia uhasama kati yake na Rais

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho wakati wa uzinduzi wa SGR Jumatano, Madaraka Express, alizuiliwa uzinduzi huo
b48a73f7300b7314dbe6647dc53b9cc0.jpg
Joho alizuiliwa na maafisa wa polisi kujiuunga na viongozi wengine katika kituo cha reli cha Miritini, akiwemo Rais Uhuru Kenyatta, aliyekuwa akizindua reli hiyo

Huenda Joho alizuiliwa baada ya kutishia kumuuliza Rais Kenyatta maswali kuhusu gharama ya utengenezaji wa reli hiyo

Joho alisema kuwa alipanga kumuuliza Rais sababu za gharama ya reli hiyo kuongezewa kwa zaidi ya Sh. 100 bilioni

Hivi majuzi wakati wa uzinduzi wa feri Mombasa Joho alizuiliwa na maafisa wa usalama
83f7641b48dd5f7fe804f7c6052cde56.jpg

Joho ni mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Jubilee hasa kuhusu masuala ya ufisadi na mradi wa SGR, amejibandika 'Adui 001' wa Uhuru Kenyatta na Jubilee

Kulingana naye, Serikali imetia kila juhudi kutetea wadhifa wake wa Ugavana Mombasa

Mgogoro kati ya Joho na Uhuru ulianza wakati Gavana huyo alipomkosoa Rais baada ya kufika Mombasa kuzindua Kivuko, alichodai hakikutengenezwa na serikali kuu ila kwa ufadhili wa Banki ya Dunia

Uhasama kati ya Joho na Rais Kenyatta huenda hautakamilika hivi karibuni, hasa msimu huu wa kisiasa, viongozi wanajipigia debe kuingia mamlakani au kuhifadhi mamlaka yao baada ya uchaguzi ujao

Naye mgombea Urais kupitia muungano wa NASA, Raila Odinga alisema, Ni makosa makubwa kwa Mkenya yeyote kuzuiwa kwa kuwa haungi mkono Serikali.
 
Kuna tofauti ya kukosoa na ujinga. Criticism and ignorance coupled with pride are two totally different things.
Tangia like boat lililokua na muhadarati kulipuliwa, joho hajakua the same again. Kisha baadaye CFS take kufungua kwa ajili ya kupitiza mizigo pasi kra kuzikagua.
 
uk ni soft sana na huyu jamaa,hana heshima
 
Back
Top Bottom