Hilo la amani sitegemei tuwe namba moja maana sisi Wakenya sio watu wa kuzimwa zimwa kama mazombi, hatupelekeshwi ovyo ovyo, huwa tupo tayari muda wowote kuhoji, tunahoji kila kitu ikiwemo historia, hatukandamizwi na kukaririshwa pumba kama mazombi kisa amani.
Hamna kitu cha ovyoo kama kutajwa unaongoza kwa amani ila watu wako wanaishi kwa kunun'gunika ndani kwa ndani, wamejaa machungu na majungu ila wanakenua meno ili tu watajwe kuwa watu wa mani. Kwa mfano utafiti unaonyesha Tanzania imetajwa ndani ya mataifa kumi ambayo wananchi wake hawana furaha hata kidogo, yaani duniani hata sio Afrika bali dunia yote mpo ndani ya mataifa kumi yenye dhiki kuu japo pia mnatajwa kama nchi yenye amani hapa Afrika......isitoshe, mnatajwa ndani ya mataifa maskini wa kutupwa duniani.
Yaani sifa ambazo sijui zinaendana kivipi, kwamba nchi ambayo watu wake wanaongoza kwa kukosa furaha duniani, ambayo imeorodheshwa ndani ya maskini wa kutupwa duniani, lakini yenye amani zaidi ya zote EAC, watu mnaishi tu muishi bila kuhoji chochote, mpo mpo tu.....https://www.fastcompany.com/90323247/these-are-the-10-happiest-and-unhappiest-countries-in-the-world-in-2019