Gavana wa Nairobi atuma Jeshi la zimamoto Kibra

Gavana wa Nairobi atuma Jeshi la zimamoto Kibra

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja, kupitia ukurasa wake wa twitter amethibitisha kutuma Zimamoto kwenda kudhibiti hali eneo la Kibra, ambapo moto mkubwa unazidi kuenea na kuteketeza nyumba za watu.

Hata hivyo Sakaja amesema kuwa awali kikosi cha Zimamoto kimeondoka shingo upande kutokana na hofu ya kushambuliwa, kwani inasadikiwa kuwa moto umeanzishwa maksudi baada ya makundi mawili kuzozana.

Maafisa wa polisi bado hawajafika Kibra, jambo ambalo limepelekea baadhi ya watu kuhisi kuwa kikundi kimoja kinafadhiliwa na Serikali kwa lengo la kumchafua Odinga kama mtu wa vurugu.
 
Back
Top Bottom