Gavana za Magari: Mradi wa nani?

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
4,526
Reaction score
1,540
Ili kupunguza ajali barabarani, Serikali ya Tanzania imeamua kuweka Gavana kwenye kila Basi na Lori eti kudhibiti mwendokasi wa Magari haya.

Lakini Barabara zetu bado ni mbovu, zina matuta kibao, mashimo kibao, hakuna sheria kali za Usalama wa Barabara kutokana na kunona kwa rushwa.

Je Mnofu huu wa Gavana za magari ni wa nani?

 
Amani Iwe Nanyi,

Iwe pia na CCM
 
Bilioni 46? Hili pande ni kubwa sana, lazima kuna mikono minene ndani yake na kama kawa wataendelea kutufyonza tu! Nakumbuka hizi gavana zilianza siku nyingi na kwenye mabasi wakalamba chao, na hivi sasa mabasi yote ylisha zinyofoa! Naona hii ni part two! tusubilie hata private car tutaletewa za kwetu lol! nchi ya CHUKUA CHAKO MAPEMA wala huta kaa uuulizwe milele.
 
Ikiwa Polisi ndio wanasukuma mradi huu kama njia kudhibiti uendeshaji magari kwa kasi, hii si ina maana kuwa Sheria za Usalama Barabarani hazina maana yeyote na Polisi wanakiri kuwa hawana uwezo kuhakikisha Madereva wanafuata sheria na hivyo suluhisho ni kuweka gavana??!!
 
Tena? Si zamani kwenye miaka ya 90 walifanyaga hivi tena...ina maana waliacha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…