Gawio la Hisa CRDB

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Kama mwanahisa napenda nielemishwe kwa yafuatayo:-

(1) Ni kigezo gani kinachotumika (Directors fees)mathalani Wakurugenzi 10 kulipwa Tshs.965,000,000 kwa mwaka na hii ina maana ya Tshs 96,500,000 kwa Mkurugenzi moja kwa mwaka na Tshs 8,041,666 kwa mwezi kwa mkurugenzi moja na kwa siku Tshs268,055 kwa Mkurugenzi moja ili hali hisa moja ni Tshs.36?

(2) Napenda kufahamu ni vikao vingapi vinavyofanyika kwa mwaka vinavyohusu Wakurugenzi?.

(3) Kwanini ajenda ya malipo ya Wakurugenzi(Directors fees) hazijadiliwi katika vikao na ajenda hii inakuja tu kama taarifa?.

(4) Kwanini vikao vya Wanahisa kila mara vinafanyikia tu Arusha? Kwanini visiwe na mzunguko mwaka huu Arusha, mwaka ujao Mbeya, mwaka unaofuata Mwanza, Dodoma nk.

Naomba majibu yangu haya yawe kwenye PRESS RELEASE ili wanahisa wote wapate kufahamu haya niliyoyauliza.
 
Hisa Moja ya CRDB ni Tsh 385 na hiyo 36 ni gawio tu ambalo mkutano Mkuu walipanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…