Gawio la shs. kwa hisa CRDB

Gawio la shs. kwa hisa CRDB

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Leo nimepewa taarifa kuwa katika kikao cha Wanahisa kilichokaa mjini Arusha imeamuliwa kuwa gawio la kila hisa iwe shs. 10. Haingii akilini kwangu kutokana na faida ya Tshs.75bn iliyopatikana gawio inakuwa shs.10 kwa hisa moja. Ninatarajia kuuza hisa zangu zipatapazo 3500 ili nichukue ustaarabu mwingine. Ina maana katika hisa zangu 3500 gawio langu ni shs.35,000 bado kodi. Kwangu naona kama tusi. Hata akaunti yangu nitahamisha kutoka CRDB.
 
du, mkuu nimewaona hapo mount meru kumbe ndo wameamua hivyo? yaani shng kumi?
 
Mkuu uwekezaji mzuri ni kununua viwanja vilivyopimwa, kwa sababu ardhi inaongezeka thamani kila siku, mimi nilikuwa na viwanja vinne hapa dar ambavyo nilivinunua miaka miwili iliyopita kwa milioni nane nimeviuza majuzi kwa milioni 40
Ni kweli kabisa mkuu hata Mimi nimeamua kufanya hvyo, huku mkoani nilipo Nina viwanja vikubwa na safi vitatu
 
Ulihudhuria hicho kikao kutoa maoni? Angalia minutes za kikao ili uweze kujua sababu ni nini zilizopeleka kuwa na maamuzi hayo!! Otherwise, it doesnt make sense kama bank inataka kufilika nyie wanahisa mnataka mgawane TZS 150 kwa kila hisa moja. Vumilia mkuu, huenda baada ya muda mambo yatakaa ingawa nayo ni gambling tu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Wewe ulinunua hisa za shilingi ngapi? maana gawio linakua ni kati ya 3% hadi 5% ya thani ya hisa ulizonunua
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Real estate ndio mpango mzima

Pia kama huna haraka,kipindi hiki watakaopaniki ni wengi na watauza sana hisa,nunua kadri ya uwezo,awamu ya tano ikiondoka madarakani na vurugu zake uchumi utasimama na unaweza ukajikuta ni mwanahisa mkubwa.

In short ,kama una hela,kipindi cha awamu ya tano kimefanikiwa kuvuruga kila kitu na kushusha purchasing power,nunua tu,ila soma mazingira,kuna kampuni nyingi bado zinasajiriwa kwa Msajili wa vifo,better get an advice
 
Juzi Tanga Cement wametangaza shs 80 kwa hisa. so kwa hisa zangu 6000 napata gawio la shs 480,000/= Hapo bado Magufuli hajachukua zake!

Hii biashara ya hisa inahitaji uvumilivu wa kipekee!
 
Mkuu uwekezaji mzuri ni kununua viwanja vilivyopimwa, kwa sababu ardhi inaongezeka thamani kila siku, mimi nilikuwa na viwanja vinne hapa dar ambavyo nilivinunua miaka miwili iliyopita kwa milioni nane nimeviuza majuzi kwa milioni 40
He, angalia usitafutwe kwa ajili ya kulipia kodi ya mapato.
 
Mkuu uwekezaji mzuri ni kununua viwanja vilivyopimwa, kwa sababu ardhi inaongezeka thamani kila siku, mimi nilikuwa na viwanja vinne hapa dar ambavyo nilivinunua miaka miwili iliyopita kwa milioni nane nimeviuza majuzi kwa milioni 40
Mkuu uko sahihi kabisa..ardhi ukitunza vizuri itakutunza zaidi....naomba kama kuna mwenye kuitaji kiwanja tuwasiliane...!
 
Aliyekwambia hisa ni asset nani? huna elimu juu ya umiliki wa hisa, huwezi kununua hisa ili kupata gawio, hisa ni kama bidhaa unaangalia asubuhi wapi inapatikana kwa bei ya chini, unanunua mchana ikipanda unauza unahesabu balance iliyobaki, unatafuta bar yenye warembo wazuri unatulia kusubiri siku nyingine. Hiyo ndi biashara ya hisa.
 
Wakati serikali inazivuruga benki tulikuwa tunachekelea,sasa ni msimu wa mavuno

" when they came for the Jews,I kept silent because I was not a Jew......"

Dunia sio mbaya kwa sababu kuna watu wabaya,bali kwa sababu watu wema wanakaa kimya wakati ubaya unafanyika........."
 
Leo nimepewa taarifa kuwa katika kikao cha Wanahisa kilichokaa mjini Arusha imeamuliwa kuwa gawio la kila hisa iwe shs. 10. Haingii akilini kwangu kutokana na faida ya Tshs.75bn iliyopatikana gawio inakuwa shs.10 kwa hisa moja. Ninatarajia kuuza hisa zangu zipatapazo 3500 ili nichukue ustaarabu mwingine. Ina maana katika hisa zangu 3500 gawio langu ni shs.35,000 bado kodi. Kwangu naona kama tusi. Hata akaunti yangu nitahamisha kutoka CRDB.
CRDB wametangaza faida ambayo ni artificial. Hawa imeripotiwa juzi juzi tu kwenye gazeti la mwananchi kuwa wamepata hasara ya bilions of money. Hii faida imetoka wapi? Kuna mtaalam kanitonya kuwa wamewrite off NPAs zao hivyo ikaregister profit. Sasa hiyo shs kumi shukuru Mungu. Benki imepata hasara kubwa mkuu. Wamefuta tu madeni ndiyo ikaonyesha faida.
 
Juzi Tanga Cement wametangaza shs 80 kwa hisa. so kwa hisa zangu 6000 napata gawio la shs 480,000/= Hapo bado Magufuli hajachukua zake!

Hii biashara ya hisa inahitaji uvumilivu wa kipekee!
Faida ya hisa siyo kwenye gawio. Ni "kuspeculate the best time to sell your shares". Faida iko kwenye mauzo. Unanunua kwa bei ndogo na unauza wakati share price imepanda.
 
Back
Top Bottom